Masaa !!! Masaa!!! Masaa!!!

Matango

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
535
Reaction score
118
Wanaotengeneza matangazo wanachangia sana kuharibu Kiswahili. Kama watu wa BAKITA na watetezi wengine wa Kiswahili wanasoma uzi huu wajitokeze kukomesha au kuwaelimisha watengenezaji wa matangazo watumie neno sahihi la SAA badala ya MASAA. Ni rahisi sana kukumbuka neno linalosikika mara kwa mara kwenye matangazo kama vile yale ya biashara. Neno lingine mtanisaidia wasomaji LISAA !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa kweli neno sahihi wingi wa saa ni saa lakini kutumia masaa limeishazoeleka na linapendeza kulitumia.
 
Ni kweli kabisa...watumiaji wa lugha wanapotosha kabisa maana na matumizi ya neno SAA. Kwa bahati mbaya Tanzania hakuna sheria inayolinda lugha ya Taifa...Kiswahili. Mtu anaweza kuitumia kwa namna yoyte ile ilimradi tu akidhi haja yake. Mfano ukitembelea kwenye matawi ya NMB utakuta kuna matangazo yamebandikwa ndani ya benki hiyo kuwaelekeza wateja utaratibu unaopaswa kufuatwa ukiwa unahitaji huduma ya kifedha: TAFADHAri SIMAMA KWENYE MSTAli neno TAFADHARI lilipaswa kuwa TAFADHALI na MSTALI lilipaswa kuwa MSTARI...lakini ni nani mwenye wajibu wa kusimamia makosa kama hayo? Ni BAKIZA au Wizara husika??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…