Ndugu wanajamii,
Mimi ni mtumishi wa umma katika taasisi fulani. Naombeni kufahamishwa Kama kuna waraka wowote wa serikali uliobadilisha viwango vya posho ya kujikimu. Mfano kumekuwa na tetesi kuwa kumekuwa na ongezeko la fedha kwa wale waliokuwa wakipata Tsh. 65,000/= na sasa wanastahili kupewa 100,000/=.
Nafahamu fika humu kuna wadau wa utawala na viongozi. Hivyo ni yangu matumaini ntasaidiwa maana kuna kazi fulani nataraji kwenda kuifanya na ntahitajika kujaza imprest. Ikumbukwe kumekuwa na michezo michafu ya watumishi kutokujuzwa mambo ya msingi kama haya yanayohusu maslahi Yao.
Aksanteni.