Masada wa kutaka kubadilisha jina la kiwanja

Saad30

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2020
Posts
2,737
Reaction score
5,464
Habari wakuu.

Mimi naombeni msaada wa kutaka kujua kama je ni kweli unaweza kubadili jina la muuzaji kiwanja kwenda kwa mnunuaji kiwanja?

Nimenunua kiwanja ambacho kina OFA tu sasa bado sjabadilisha jina na nyaraka zote ninazo ambazo kanipa muuzaji sasa nikaongea na afsa ardhi kaniambia hapo tunabadilisha jina bila wasiwasi kwenda kwenye hati ya kiwanja kabisa na jina linasoma lako (mimi mnunuaji) kwahiyo isikusumbue hata kama huyo aliyekuuzia hayupo au yupo bize na mambo mengine tunabadilisha moja kwa moja kwenda kwenye HATI ya kiwanja.
 
Fuata taratibu utakuja kunishukuru. Usikubali short-cut
 
Kama hakuwa na hati basi unabadili tu majina kwenye zile documents za wapimaji hati inatoka kwa jina lako.
 
Vipi kukiwa na hati mkuu.. nataka ninunue eneo lina hati ,vitu gan vya msing nizingatie kabla sijampa mpunga wangu,na vinahitajika kwenye kubadili jina
 
Sijawahi kununua eneo lenye hati mkuu ila nadhani cha muhimu uende kuconfirm kama hati ni halisi na anaeuza ni mmiliki halali.

Fuata hatua zote muhimu na salama kwa manunuzi ikiwamo kuwashirikisha majirani wa eneo husika na kuhakikisha unatumia mwanasheria kusimamia mkataba wa manunuzi husika.
Ahsante.
 
Shukran mkuu
 
Back
Top Bottom