Masahihisho: Historia ya African Association Kama Ilivyoelezwa Katika Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma

Masahihisho: Historia ya African Association Kama Ilivyoelezwa Katika Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074

View: https://youtu.be/X8aFsrqOgUQ?si=_R7PLruw4fYbQTWK

Historia ya African Association imekosewa kidogo.

African Association inachanganywa na Tanganyika African Association (TAA).

African Association ilibadili jina na kuwa Tanganyika African Association (TAA) mwaka wa 1948 kujitofautisha na African Association ya Zanzibar.

Hii historia ya kuasisiwa kwa African Association iliandikwa na Kleist Sykes kwa mkono wake mwenyewe kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Huu ulikuwa mswada wa kitabu na alikuwanao Abdul Sykes hadi mwaka wa 1968.

Mwaka wa 1968 Aisha "Daisy" Sykes mtoto wa Abdul Sykes akiwa mwanafunzi wa University of East Africa alipewa kazi na mwalimu wake John Iliffe aandike historia ya babu yake Kleist Sykes kama seminar paper katika History Department.

Abdul Sykes akampa Daisy ule mswada ulioandikwa na babu yake.

Kutokana na mswada huu ndiyo Daisy akaandika maisha ya Kleist Sykes na kueleza yote yaliyoandikwa na babu yake.

Kleist Sykes alikutana na Dr. Kwegyir Aggrey mwaka wa 1924 na Dr. Aggrey akamshauri Kleist aunde African Association.

African Association ikaundwa mwaka wa 1929 na waasisi ni hawa: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Rawson Watts na Raikes Kusi.

Hii seminar paper iko History Department Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam hadi hii leo.

Haikuishia hapo.

John Iliffe akaitia kama sura katika kitabu alichohariri: "Modern Tanzanians," (1973).

Historia hii ipo kwa ukamilifu wake katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
 
Historia ya Tanganyika inapaswa iandikwe upya. Mzee Said natumaini umeandika kitabu na itokee na waandishi wengine watuandalie vitabu vyenye utajiri wa historia ya uhuru wetu wa Tanganyika

Ninahoja pia kuhusu huyo MC mzee Kisu. Yeye kila mara hawapi nafasi wasemaji kumalizia points zao anawahimiza wamalizie haraka kuongea na huwa hafuatilii wanachokiongea. Ni aina ya watu ambao hujipa hekaheka kwenye shughuli isiyo yao. Hapo amemtoa mzungumzaji kabla hajamalizia points zake
 
Kabisa maana kuna wanasiasa wanaipindisha ili ku favour interest zao za sasa
 
Back
Top Bottom