Masai wakatazwa kutembea na fimbo Zanzibar; Je, Wamasai wamewakosea nini kila sehemu mnawakataa?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Masai ni jadi yake kutembea na fimbo miaka yote. Hakuna siku tumewahi kuiona fimbo ya Masai kama silaha. Kinachoendelea Zanzibar ni mwendelezo wakupambana na kabila hili kutokana na ukweli kwamba wamejaa Zanzibar na wanaongea vibaya kuhusu ngorongoro.

Ukiwakuta wakiwa na wazungu wanajadili mada ya Ngorongoro na matamshi yao ni wazi siyo mazuri. Pamoja na matamshi mabaya dhidi ya wenzetu, haikuwa na tija kuwapelekea askari wawapige. Wamepigwa na wao ni binadamu wakapiga. Leo limetolewa tamko hakuna ruhusa Masai kuingia zenji na fimbo wala sime......je sheria gani imetamkwa haya?

Lakini wazungu wanatembea uchi Zanzibar na hakuna askari anayewagusa....wanatembea na dogs hakuna makatazo. Wanafanya mengi mabaya lakini tupo kimya....Masai kuonekana kero ngorongoro na sasa kero Zanzibar . Tulitegemea afuge mifugo na kuishi maisha duni tumtawale ? Ameamua kujitawala.

Natambua mahakama Zanzibar itawafunga miaka mingi tena ndani ya muda mfupi ujao.....lakini one day watakuwa huru
 
Mkoloni Mweupe mwenyewe alikuwa akiwaruhusu Wamasai kutembea na fimbo virungu na sime zao.

Huyu Mkoloni Mweusi ni katili zaidi.
 
Kinachoendelea Zanzibar ni mwendelezo wakupambana na kabila hili kutokana na ukweli kwamba wamejaa Zanzibar na wanaongea vibaya kuhusu ngorongoro.
Chukua ujumbe wako!

punguani

/punguwani/

mtu aliyepungua akili

-enye kupungua au kuwa pungufu

Akili punguani

Hivi hawa wamasai kweli au wahuni flani tu wamejivisha mavazi ya kimasai🤣🤣
 
Sasa sime na bakora za nini zenji?Hakuna kuchunga wala kuwinda zanzibar.Hayo mavitu alafu jamaa zetu wakipandisha mori lazima damu imwaike.
 
Huyu mama Samia ni shetani.

Anaruhusu unyama dhidi ya wamasai.

Aende kuzimu na chuki zake.
 
Masai ni jadi yake kutembea na fimbo miaka yote. Hakuna siku tumewahi kuiona fimbo ya Masai kama silaha. Kinachoendelea Zanzibar ni mwendelezo wakupambana na kabila hili kutokana na ukweli kwamba wamejaa Zanzibar na wanaongea vibaya kuhusu ngorongoro.

Ukiwakuta wakiwa na wazungu wanajadili mada ya Ngorongoro na matamshi yao ni wazi siyo mazuri. Pamoja na matamshi mabaya dhidi ya wenzetu, haikuwa na tija kuwapelekea askari wawapige. Wamepigwa na wao ni binadamu wakapiga. Leo limetolewa tamko hakuna ruhusa Masai kuingia zenji na fimbo wala sime......je sheria gani imetamkwa haya?

Lakini wazungu wanatembea uchi Zanzibar na hakuna askari anayewagusa....wanatembea na dogs hakuna makatazo. Wanafanya mengi mabaya lakini tupo kimya....Masai kuonekana kero ngorongoro na sasa kero Zanzibar . Tulitegemea afuge mifugo na kuishi maisha duni tumtawale ? Ameamua kujitawala.

Natambua mahakama Zanzibar itawafunga miaka mingi tena ndani ya muda mfupi ujao.....lakini one day watakuwa huru
Acha hizo hapa Dar es salaam wanatembea wakiuza dawa zao,viatu,shang's,nail clippers bila sime Wala marungu.
Wstoke kwenye ujima sio kila mahali ni Ngorongo kwenye wanyama wakali
 
Kwa hiyo wewe mkazi wa kinondon unafikiri sime na mapanga kwa wamasai ni sababu ya wanyama wakali?
 
Back
Top Bottom