Masanduku ya Kura yakamatwa Sunday, 31 October 2010 14:04
Mwananchi
Israel Mgussi na Geroda Mabumo ,Dodoma
HALI ya uchaguzi mkuu jimbo la Dodoma mjini imetia dosari baada ya kukamatwa kwa masanduku ya kupigia kura yakiwa na karatasi za kura kwenye nyumba ya mtu binafsi nje kabisa na kituo cha kupigia kura.
Masanduku hayo mawili yaliyokuwa yamesheheni karatasi za kura ndani yalikamatwa juzi mtaa wa Majengo mjini Dodoma majira ya saa mbili usiku kwenye nyumba ya Mwalimu Walburga Tarimo ambaye pia ilifahamika kuwa ndiye atakayekuwa msimamizi wa kituo cha uchaguzi cha Makole kata ya makole.
Mwananchi ambayo ilifika eneo la tukio ilishuhudia upekuzi ulioongozwa na Afisa upelelezi makosa ya jinai wa wilaya ya Dodoma mjini(OC-CID) Jonathan Shanu ambapo masanduku hayo mawili yalibainika na kuchukuliwa moja kwa moja hadi kituo cha polisi cha kati pamoja na mtuhumiwa kwa ajili kutolea maelezo.
Baada ya kufika kituo cha polisi cha kati masanduku yalifunguliwa ili polisi na mashuhuda waweze kujiridhisha kama karatasi zilizokuwamo ndani zilikuwa zimeshawekwa alama zinazoonyesha kuwa kura zimeshapigwa au hapana.
Hata hivyo baada ya masanduku hayo kufunguliwa karatasi zilizokuwamo ndani zilikutwa bado hazijatiwa alama ya vema wala alama yoyote inayoonyesha dhamira ya kumpigia mtu fulani kura na zaidi ya hapo mtuhumiwa alisema kuwa yeye alilazimika kurudi na masanduku na vifaa vyote vya kupigia kura kutokana na kukosekana kwa ulinzi katika kituo cha kupigia kura.
Mimi sikufahamu kuwa hili ni kosa na nililazimika kurudi na vifaa vyote hivyo vya kupigia kura kwa sababu giza lilishaingia katika kituo cha kupigia kura na hapakuwepo na ulinzi wowote wa askari hivyo kwa usalama wangu na wa vifaa niliamua kurudi navyo nyumbani.,alisema mwl.Tarimo ambaye ndiye msimamizi wa kituo cha uchaguzi Makole .
Haikuweza kufahamika sababu ambazo zilifanya mtuhumiwa ashindwe kuwasiliana na msimamizi wa uchaguzi au kwa vyombo vingine vya usalama ingawa ilibainika kuwa katika kituo husika kulikuwepo na askari ambaye alikuwa amepangwa kutoa ushirikiano wa kiulinzi na usalama katika kituo tajwa.
Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Dodoma mjini Suzane Bidya alisema yeye hana taarifa juu ya kukamatwa kwa masanduku hayo na kusisitiza kuwa hakuna sheria inayomruhusu mtu yoyote kwenda kulala na vifaa vya uchaguzi nyumbani kwake.
Mimi sina taarifa hizo,hata hivyo muulize huyo mama nani kamruhusu kwenda na masanduku na hivyo vifaa vya kupigia kura nyumbani kwake,akueleze maana mimi sijatoa ruhusa hiyo na wala sina ruhusa ya kumruhusu mtu kwenda na vifaa vya kupigia kura nyumbani kwake sasa yeye kwanini aende navyo nyumbani.,alisema Bidya.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Steven Zelothe alipotakiwa azungumzie tukio hili alisema kuwa hakuna taarifa inayohusu tukio hilo ambayo imeshamfikia.
Aidha baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na kufanyika kwa uhakiki wa karatasi zilizokuwemo ndani ya masanduku hayo,yalichukuliwa na kupelekwa kwenye kituo husika cha kupigia kura chini ya ulinzi wa polisi,huku OC-CID Dodoma mjini Jonathan Shanu akisema kuwa maelezo yameshachukuliwa lakini yeye hawezi kutoa maelezo yoyote kwa sababu yeye sio msemaji wa Polisi.
Mbali na dosari hiyo upigaji kura katika vituo mbalimbali vya majimbo ya Dodoma mjini,Bahi na Chamwino imeendelea vizuri huku kukiwa na hali ya utulivu na upigaji kura wa amani.