Masanja Awaangukia Polisi, amaliza msala wa kuvaa sare zao

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253


Katika harusi ya Masanja Mkandamizaji iliyofanyika Agosti 14, wachekeshaji wenzake wa kundi la Orijino Komedi, walikuja wamevalia nguo zilizofanana na sare za jeshi la Polisi hali iliyowapelekea kukamatwa. Walifikishwa kituo cha Polisi kwa mahojiano na pia wakakaguliwa sehemu wanazoishi ili kuweza kufahamika kama kuna kitu kingine wanachomiliki tofauti na sare za Polisi.

Kufuatia hatua hiyo, Masanja Makandamizaji ameandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Facebook kwenda kwa mashabiki wao wanaoulizia kuhusu hatma ya wachekeshaji hao waliokuwa wanashikiliwa na Polisi.

“Jamani asanteni kwa maombi yenu na meseji zenu za kuulizia juu ya ishu ya Polisi, tunamshukuru Mungu tumewaomba msamaha na wametusamehe hivyo imekwisha.

Tumesema tulinogewa na harusi tukasahau kwenda kuomba kibali. Lakini wakina Joti, Seki, Mac Reagan na Wakuvanga wamepata kautamu ka mahojiano. Ishukuriwe honeymoon imeniokoa mwee na mimi ningekuwa kwenye jiji la Makonda ingenihusu.

Hii ilikuwa karibu Monica maana alishaanza kupata presha, eti ananiuliza na wewe ukirudi utaenda Central, nikasema sio mimi tu, ni mimi na wewe.”
 
Walizipata wapi hizo nguo zinazokaribia kufanana na sare ya polisi japo haikuwa sare kamili?!!
 
Sheria inaruhusu kusamehewa bila kufikishwa mahakamani?
Kuhojiwa siyo kigezo cha kuwa na hatia, au unatamani kupoteza tuu pesa za serikali kuendesha kesi zisizo na msingi?
 
Nachodhani! Ni kwamba masanja kamchekesha mkubwa mmoja huko akacheka mpaka mbavu zikamuuma akatoa amri hebu waachieni hao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…