Kwanza kabisa niwatakie Jumatatu ya Pasaka yenye Baraka
Sasa naomba majibu ya swali langu
Masanja Kadogosa ni Katibu wa Bodi ya TRC na anaingia Hapo siyo kwa kuteuliwa bali kutokana na Cheo chake cha Mkurugenzi mkuu wa TRC
Sasa Masanja Mkandamizaji katumbuliwa kwenye Bodi je bado ana uhalali wa kuendelea kuwa MD na ikiteuliwa Bodi nyingine arudi tena kama Katibu?
Nipo hapa kuelimishwa
Shujaa : Nitawaletea Treni ile Watoto wa Mjini wanaiita " Mjusi"
Yes yeye anaendelea kwasababu yeye ni mtu safi, hahusiki ila najua kuna watu wana hamu sana Wasukuma wote walioteuliwa na Magufuli, watumbuliwe kwasababu wanadhani waliteuliwa kwa Usukuma wao na sio kwa sifa zao na vigezo.
Mama akifanya kosa hili, la kuwatumbua Wasukuma kwasababu tuu ni Wasukuma na waliteuliwa na Msukuma, atakuwa anatenda dhambi kubwa ya ubaguzi!. Japo Rais Magufuli ni Msukuma, sijui ni wangapi humu wanafahamu kwanini ni Magufuli, Mimi ni mmoja wa watu wachache sana wanafahamu why ni Magufuli
https://www.jamiiforums.com/threads...ccm-2015-could-be-john-pombe-magufuli.707165/
Na japo Magufuli alijaza Wasukuma baadhi ya maeneo, niliwahi kulishauri Bunge letu lichunguze
https://www.jamiiforums.com/threads...bu-na-zile-boeing-ni-tt-then-hatufai.1246099/
Hivyo japo ni kweli Magufuli aliwateua Wasukuma wengi lakini hakuwateua kwa sababu ya Usukuma wao, aliwateua kwasababu ya kukidhi sifa na vigezo
https://www.jamiiforums.com/threads...enye-ukabila-tatizo-ndio-walio-wengi.1290353/
Hivyo Mama akifanya kosa la kuwatumbua Wasukuma kwa Usukuma wao, atakuwa amefanya kosa kubwa la dhambi ya ubaguzi, karma haitamuacha Mama salama!.
Japo hakuna mtu yoyote ajuaye ni kwanini JPM ameitwa mapema, lakini wapo watu wanaojua na sababu wanazijua, hivyo wana jukumu la kumsaidia Mama kuepuka mambo yanayotengeneza bad karma
Inabidi kwenye vile vikao kazi vyao na semina elekezi wawe wanaita na watu wa holistic advice ili wafundishwe kitu kinachoitwa karma, it's real na kuhakikisha wanapoboronga, wanapisha tuu wenyewe ili kumlinda Mama
https://www.jamiiforums.com/threads...shia-rais-wetu-kubeba-mzigo-wa-karma.1946897/
P