Masanja Kadogosa: Kukatika kwa umeme hakutakwamisha utendaji wa Reli ya SGR

Masanja Kadogosa: Kukatika kwa umeme hakutakwamisha utendaji wa Reli ya SGR

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Mkurugenzi wa Shirikla la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa wakati anazungumza na kutoa maelekezo kabla ya safari ya kutokea Dar - Moro mapema leo, Februari 26, 2024.
Snapinsta.app_429907418_795767822590947_4582168767238296139_n_1080.jpg

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza majaribio ya Treni ya Umeme ya Kisasa ya (SGR) kutoka Mkoani Dar es Salaam hadi Morogoro huku ikielezwa kuwa Huduma rasmi za Usafiri huo zinatarajiwa kuanza Mwezi wa Julai, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TCR), Masanja Kadogosa amewataka Wananchi waondoe hofu kuhusu tatizo la kukata umeme katika safari za treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kuwa reli hiyo ina mkondo wa umeme unaojitegemea.

Kadogosa amesema hayo Februari 26, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa safari ya majaribio ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

"Tuna mkondo unaojitegemea kwa ajili ya reli tu, hatuingiliani na mtu yeyote, na mkondo huo umeunganishwa kwenye gridi kubwa na vyanzo vyote vya umeme ndani ya nchi hii," amesema Kadogosa.

Pia, amesema kuunganishwa kwa reli hiyo katika vyanzo vyote vya umeme vilivyoko nchini ni tafsiri kwamba haiwezi kukwama kwa sababu ya kukatika umeme.
 
Wenye mabasi watulie wasijaribu kuhujumu reli hiyo. Mabasi yao nayo yatapata wateja wake
 
Vyanzo vyote vya umeme nchini ni vipi, mbona kama hayuko huru?
 
Ninachojua treni ni la diesel si la umeme. Waache siasa bhana.
 
Back
Top Bottom