Masanja Mkandamizaji ashangazwa na Serikali kupunguza faini EFD, adai ni kuruhusu wafanyabiashara kufanya makosa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Pastor Masanja akiwa kwenye kipindi kwenye redio ya EFM ameipongeza TRA kuongeza makusanyo kwa 14.5% kufikia trilioni 27.64 kwa mwaka wa fedha 2023/24 lakini amesikitishwa na uamuzi wa Serikali kupunguza faini ya kutotoa risiti ya EFD kwa wafanyabiashara kutoka milioni 15 mpaka milioni 4.

Masanja amesema Serikali haitaki wafanyabiashara walipe faini, amewasihi kufanya biashara kihalali wasikutane na faini.

Masanja Mkandamizaji.jpeg

Masanja amesema wanapolalamika faini kubwa na kutaka faini ndogo inamaanisha wanataka kuendelea kufanya makosa.

Masanja amehoji kwanini mtu apunguziwe adhabu ya kosa ambalo bado hajafanya.
 
Nani atalipa M15 sababu hajatoa risiti ya 200,000/=? Ni kutengeneza mazingira ya rushwa tu hakuna pesa itaenda serikalini. Hata M4 ni kubwa, wangeweka 100% ya kodi iliyokwepwa na 10% interest..
 
Nimekubali hoja yako 💯
Kumbe fain ya EFD ilikuw 15M , hiiz fain ziliandaliw na wataalamu kbs?
 
Kuna wakati saa mbivu hutoa muda sahihi. Masanja yuko sahihi.

Kwa nini wafanyabishara walalamikie adhabu ya 15m ni kubwa kwa kutokutoa risiti? Lengo lao la kutaka hiyo adhabu ipunguze ni nini?
Haina uhalisia. Makosa yapo tu yanatokea ndo maana fain zinawekwa. Unaweza ukatoa risiti kwa 99% ila ukatoka kidogo mfanyakazi wako akajisahau asitoe, au hata wewe katika kuhudumia labda wateja wengi mtu kanunua kitu cha elfu tano ukampa ukaanza kumsikiliza mwingine na hujampa wa elf tano risiti. Chukulia mfano makosa ya barabarani uambiwe ukipita kwenye taa fain laki tano, nani atalipa?
 
Kuna wakati saa mbivu hutoa muda sahihi. Masanja yuko sahihi.

Kwa nini wafanyabishara walalamikie adhabu ya 15m ni kubwa kwa kutokutoa risiti? Lengo lao la kutaka hiyo adhabu ipunguze ni nini?
Lengo lao wasitoe risiti ili walipe adhabu ndogo kwa kuwa wanapata faida kubwa kwa kuwaibia maskini.
 
Pastor Masanja akiwa kwenye kipindi kwenye redio ya EFM ameipongeza TRA kuongeza makusanyo kwa 14.5% kufikia trilioni 27.64 kwa mwaka wa fedha 2023/24 lakini amesikitishwa na uamuzi wa Serikali kupunguza faini ya kutotoa risiti ya EFD kwa wafanyabiashara kutoka milioni 15 mpaka milioni 4.

Masanja amesema Serikali haitaki wafanyabiashara walipe faini, amewasihi kufanya biashara kihalali wasikutane na faini.

Masanja amesema wanapolalamika faini kubwa na kutaka faini ndogo inamaanisha wanataka kuendelea kufanya makosa.

Masanja amehoji kwanini mtu apunguziwe adhabu ya kosa ambalo bado hajafanya.
Wazalendo Bado tupo wachache sana, hongera bwana masanja
 
Ndio shida ya kuruhusu wasio na shule kujifanya wanajua kushinda wenye shule sababu wenye shule wameshindwa kutetea wasio na shule wakabaki kutetea matumbo yao na kufanya wasio na shule kujiona nao wana shule zaidi ya wenye shule.

Nadhani nimeelekweka. Asante.
 
hakuna anaelipishwa faini milioni 15, bali kinachofanyika hapo ni kulazimishwa kutoa rushwa ya hela ndefu. kadri itakavyo pungua ndivyo rushwa itakavyopungua
 
Back
Top Bottom