Masao Bwire: Ruvu Shooting itatwaa Ligi Kuu Msimu Ujao

Masao Bwire: Ruvu Shooting itatwaa Ligi Kuu Msimu Ujao

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Yule msemaji mahiri kabisa katika soka la bongo, Masao Bwire wa Ruvu shooting ameanza tambo zake mara baada ya timu yake kurudi ligi kuu na kuhaidi kuwa timu hiyo ya RUVU shooting itatwaa ubingwa msimu ujao kwani wao ndio watakuwa Leicester City ya bongo.

Wamejipanga vya kutosha kuja kutwaa ubingwa huo unaoshikiliwa na Yanga. Huyo ndio masao bwire, msenaji bora kabisa wa klabu za kibongo, hao akina Jerry Muro na Manara wajiandae...
 
Timu pekee iliyowahi kuleta maajabu Tanzania ni Tukuyu Stars tu. Afu cha ajabu baada tu ya kubeba kombe ikashuka daraja
 
Masau anazungumza vizuri na kwa utulivu mkubwa. Wasemaji wengi wana nafasi kubwa ya kujifunza.
 
Bado tu safari ndefu kweli. Timu za Ulaya wasemaji wanakuwa makocha na wale wa benchi la ufundi, ambao wanaijua timu na wachezaji wao vizuri. Huku hata makamu mwenyekiti anazungumzia timu tena katika suala la kitaalamu ambalo kocha ndiye anatakiwa kulitolea ufafanuzi.
 
Huyu jamaa namwona ni copy paste ya Thobias Kifaru wa Mtibwa.
 
Back
Top Bottom