Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
Anaandika Mo Mlimwengu.
Historia hutusaidia kujua tulipotoka, tulipo na tunapoenda. Mh Geofrey Mwambe Mbunge wa Masasi Mjini anazidi kujipambanua kiutendaji namna ambavyo anajitahidi kusukuma maendeleo kwenye jimbo lake.
Binadamu tumeumbwa kusahau na kuna wakati mtu akifanya mazuri tunaona ni kama wajibu wake. Wana Masasi wamezoea kuyaona mazuri yanayofanywa na Mwambe hivyo wanaweza kuyachukulia kawaida na kuona kama ndio wajibu wake. Tukisema ukweli Mwambe anahitaji kupongezwa kutokana na umahiri wake wa kutatua matatizo ndani ya Masasi.
Mwenye masikio atasikia na mwenye macho ataona kwa kasi ambayo anaitumia kwenye kuleta maendeleo. Mwambe kaamua anahakikisha kuboresha ustawi wa jamii wa Masasi . Ni Mwambe huyu huyu ambaye juzi tulishuhudia akigawa magari matatu kwenye shule za sekondari za Marika ,Sululu na Temeke. Lengo mahsusi ni kutoa motisha kwa walimu na hii itasaidia kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi.
Jamii ya watu wa kusini kilio kikubwa ni kutokuwa na elimu lakini unaona ambavyo Mwambe kaamua kulivalia njuga suala la elimu. Amekuwa akitumia nafasi yake ya ubunge kushawishi taasisi kusaidia suala la elimu. Tumeona ambavyo amekuwa akivutia taasisi kibao kama NMB, Vodacom kutoa ufadhili kwenye masuala ya elimu na afya.
Kwa Masasi tunaweza kusema Mwambe amekuwa game changer, ni mwanasiasa ambaye siasa zake kazielekeza kwenye utendaji zaidi kuliko kuzungumza tu kama ilivyozoeleka. Leo hii waislamu wa Masasi wanajivunia kuwa na Mwambe kwa kitendo cha kuhakikisha anafanikisha kupata mfadhili wa kuwajengea msikiti ambapo gharama yake ilikuwa milioni 500. Lakini ushawishi wake na moyo wake alifanikisha kumpata Bakhresa kufanya ufadhili huo. Mwambe kaamua kutumia akili na nguvu zake kuwapambania wana Masasi. Leo hii ndani ya Masasi kuna mabadiliko makubwa sasa hivi barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami na huku vijijini barabara zinazidi kuboreshwa. Serikali ya awamu ya sita ya Mh Samia Suluhu Hassan imempata mwakilishi mzuri ndani ya Masasi mjini.
Huduma za kijamii zinazidi kuboreshwa ,zahanati zinajengwa. Hospitali ya Mkomaindo tumeshuhudia ikipokea vifaa tiba vya thamani ya mamilioni ambavyo vinasaidia kutoa huduma kwa ufasaha. Hospitali inaboreshwa na huku huduma ambazo awali zilikuwa hazitolewi zimeanza kutolewa baada ya Mwambe kuchukua jimbo.
Tumeona namna ambavyo amewatua ndoo wakina mama kwenye suala la maji. Kitongoji cha Ipiho Kata ya Marika kwa sasa wana maji ya kutosha ambapo ilikuwa haijawahi kutokea. Ukienda kijiji cha Chakama kata ya Matawale nako umejengwa mradi mkubwa wa maji kwa kushirikiana na Ruwasa ambao utasaidia wananchi kufaidika na maji. Suala la maji kilikuwa ni kilio cha muda mrefu lakini kwa sasa wananchi wananufaika na matunda ya serikali ya awamu yao ya sita.
Mwambe amekuwa tafsiri halisi ya kiongozi ndani ya Masasi. Akiahidi anatekeleza na amekuwa kiongozi mzuri wa kutatua yale ambayo miaka yote yalishindwa kutatuliwa. Na ni kiongozi ambaye anahakikisha kila sekta inafanya kazi vizuri. Amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wakulima wa mikoa ya kusini wananufaika na zao la Korosho lakini mbali na hilo hata kwenye michezo amekuwa mstari wa mbele. Tuliona namna ambavyo amejitolea kuisaidia timu ya Mkuti Market Fc kwa vifaa vya michezo na gharama nyingine walipochukua ubingwa wa mkoa. Kwa sasa Mh Geofrey Mwambe amekuwa nembo halisi ya wana Masasi kutokana na kazi ambazo anazifanya kwenye jimbo lake.
Kwa hii miaka miwili ya ubunge wake ndani ya Masasi kashafanya vitu vingi. Kwa kasi hii baada ya miaka mitano tunaiona Masasi kama Dubai kama alivyosema awali wakati anachukua kijiti cha ubunge. Wana Masasi kwa Mwambe walilamba dume na hii itapelelekea Masasi kukimbia zaidi kimaendeleo.
1 NOVEMBER 2022