Maseneta 100 wa Marekani waapishwa kama Baraza la mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Maseneta 100 wa Marekani wameapishwa Alhamisi kama baraza la mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump.

Hakimu mkuu wa mahakama ya juu zaidi John Roberts aliapisha maseneta kuhakikisha wanatenda haki bila upendeleo.

Wiki zijazo, maseneta wataamua iwapo Trump anastahili kuondolewa madarakani kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi.

Kesi hiyo imepangiwa kuanza kusikilizwa Januari 21.

Hakimu Roberts aliwauliza maseneta, " Je mnaapa ya kwamba katika kesi inayomkabili Donald Trump, Rais wa Marekani, ambayo inayongoja kusikilizwa, mutatenda haki bila upendeleo kulingana na katiba, Mungu awasaidie?"

Wabunge wakajibu "Ndio" kabla ya kila mmoja wao kusaini kitabu walichochukulia kiapo. Kiongozi wa waliowengi wa Republican Mitch McConnell, kisha akaahirisha kikao cha kutathmini iwapo Donald Trump ana kesi ya kujibu na kutangaza kwanza kesi hiyo itaanza kusikilizwa Jumanne, 13:00 EST (18:00 GMT).

Bwana Trump anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka na kuingilia bunge. Hata hivyo amekanusha kutekeleza makosa hayo na kusema kwamba kesi dhidi yake ni madai dhidi yake ni ya uongo

Kilichotokea Alhamisi?
Vikao vya bunge la Seneti vilianza huku msimamizi wa bunge akihakikisha shughuli za bunge ziko sawa (sergeant at arms). Vifungu vya kumuondoa Trump madarakani vilisomwa na mbunge wa Congress na mwendesha mashtaka mkuu Adam Schiff.

Bwana Schiff ni mmoja kati ya watu saba ambao watakuwa wanafanya maamuzi ya kesi dhidi ya Rais. Alisema hakuna Rais ambaye amewahi kuzuia mchakato wa kura ya kutokuwa na imani naye.

Chuck Schumer, Kiongozi wa Democratic katika bunge la Seneti, alitoa tena wito kwa mashahidi wapya kujitokeza na vilevile ushahidi wa nyaraka uruhusiwe bungeni. ''Kesi hii inahitaji uthibitisho wa wazi.''

Bunge la Wawakilishi limemshtumu Rais kwa kujaribu kumkandamaiza kiongozi wa nje kwa manufaa ya kibinafsi," Schumer amesema.

Spika wa Bunge Nancy Pelosi ametaka mchakato wa kesi kufanyika kwa haki
Seneta Susan Collins wa Republican ambaye atakuwa na kibarua kigumu cha kuchaguliwa tena mwaka huu, alionekana akibubujikwa na machozi wakati mashtaka yanasomwa.

Wabunge waandamizi wa Democrats walimkosoa pakubwa McConnell baada ya kuahidi kushirikiana na Rais Trump na kuonekana kama anatengua kiapo walichoapishwa maseneta wa Republican cha kuendeleza kesi hiyo kwa haki na bila upendeleo.

Akizungumza baada ya vikao vya Alhamisi, Bwana Schumer aliwaambia wanahabari: "McConnell amesema kwamba yeye atashirikiana na Rais, sisi hatutashirikiana na yeyote."

Schumer amesema anatarajia kwamba wiki ijayo kutapigwa kura ya iwapo mashahidi wataitwa na kuongeza kuwa hajaona azimio la kiongozi wa wabunge wa Republican kuhusu sheria za kufuatwa wakati wa kesi hiyo.

Bwana McConnell hajaondoa uwezekano wa mashihidi kuitwa. Lakini alipendekeza kwamba hilo litakuwa ni sawa na kuigiza kesi ya kutokuwa na imani ya Rais Bill Clinton 1999, wakati ambapo maseneta walipiga kura ya mashahidi watakaoitwa na kufuatiwa na majadiliano makali na kipindi cha maswali yaliyoandikwa.

Nancy Pelosi
Wakati kikao hicho kinaelekea kukamilika katika eneo la Capitol Hill, Alhamisi, Trump aliwaambia wanahabari waliokuwa Ikulu kwamba kesi hiyo inastahili kumalizika haraka iwezekanavyo.

"Huu ni uwongo mtupu," Rais amesema. "Madai ya undanganyifu yaliyotungwa na Democrats ili wapate kushinda katika uchaguzi." Alirejelelea kauli yake kwenye mtandao wa Twitter na kusema kwamba amefunguliwa kesi ya kumuondoa madarakani kwa kupiga simu ya nia njema.

Kiongozi wa bunge la Seneti kwa kutoka Democratic Chuck Schumer

Nini kilichotokea?
Democrats wanadai kwamba Rais alizuia $391m (£299m) msaada wa kijeshi ili kushinikiza Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa, Joe Biden. Trump ni Rais wa tatu kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye. Marasis wawili wa kwanza ni Andrew Johnson na Bill Clinton ambao hawakuondolewa madarakani.

BBC
 
United States the most democratic country in the world! Ingekuwa kule kwingine sijui ungeanzaje au japo kuwa na wazo tu la "kutokuwa na imani" na His Holiness the Supreme Grand Leader? Yaani unaanzaje kuwaza kutokuwa na imani na The One Whose Words Are The Final? Utararuliwa vipande vipande wala kaburi lako halitaonekana milele na milele. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni - Marekani wana demokrasia sana.
 
Democracy na maendeleo ya nchi inahitaji watu wenye msimamo... mimi sio mUS lakini namuunga mkono Nansi pelosi laiti Tanzania tungepata wanasiasa jasiri wanaojali masilahi na maendeleo ya kisiasa, na kijamii, na yote huleta maendeleo ya kiuchumi. Hakuna maendeleo pasipokua na uwazi.
 
i

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Clinton kulikuwa na ushahidi wa wazi kabisa kuwa alikuwa anambandua Lewinsky ofisin lakini hawakumwondoa madarakani. Bado nawaza hapa watatumia njia gani?

Sent using Jamii Forums mobile app

Kilichombeba Clinton ndicho huenda kikaenda kumbeba na Trump awamu hii,nacho ni wingi wa wajumbe wa chama chake kwenye bunge la seneti ambalo ndilo litafanya maamuzi ya mwisho.

Hoja inayobaki ni je,rais Trump yuko vyema na maseneta hawa kiasi cha wao kuamua kukibeba chama kama wale wa Democrats walivyoamua kukibeba chama kwa Clinton?

Ikumbukwe, mazingira yaleyale ya Clinton miaka hiyo (chama cha upinzani kuwa wengi kwenye congress yanakoanziaga mashitaka) ndivyo ilivyo sasa kwa Trump huku upande wa waamuzi (seneti) wakipamiliki chama tawala.

Ni suala la kuupa muda nafasi, japo kwangu mimi naona kabisa Trump akipeta na kubaki madarakani hadi uchaguzi wa mwaka huu hapo Novemba.
 
Democracy na maendeleo ya nchi inahitaji watu wenye msimamo... mimi sio mUS lakini namuunga mkono Nansi pelosi laiti Tanzania tungepata wanasiasa jasiri wanaojali masilahi na maendeleo ya kisiasa, na kijamii, na yote huleta maendeleo ya kiuchumi. Hakuna maendeleo pasipokua na uwazi.
Sure! Demekrasia na uwazi vichukue nafasi yake.
 
Kilichombeba Clinton ndicho huenda kikaenda kumbeba na Trump awamu hii,nacho ni wingi wa wajumbe wa chama chake kwenye bunge la seneti ambalo ndilo litafanya maamuzi ya mwisho.

Hoja inayobaki ni je,rais Trump yuko vyema na maseneta hawa kiasi cha wao kuamua kukibeba chama kama wale wa Democrats walivyoamua kukibeba chama kwa Clinton?

Ikumbukwe, mazingira yaleyale ya Clinton miaka hiyo (chama cha upinzani kuwa wengi kwenye congress yanakoanziaga mashitaka) ndivyo ilivyo sasa kwa Trump huku upande wa waamuzi (seneti) wakipamiliki chama tawala.

Ni suala la kuupa muda nafasi, japo kwangu mimi naona kabisa Trump akipeta na kubaki madarakani hadi uchaguzi wa mwaka huu hapo Novemba.
... ile kashfa ya Clinton ilikuwa mbaya na ya aibu kuzidi hii case ya Trump kwa viwango vyovyote vile. Kama Democrats walimbeba "mtu wao" kwa uchafu ule itakuwa ajabu kwa Republicans kutombeba Trump for "no issue".
 
United States the most democratic country in the world! Ingekuwa kule kwingine sijui ungeanzaje au japo kuwa na wazo tu la "kutokuwa na imani" na His Holiness the Supreme Grand Leader? Yaani unaanzaje kuwaza kutokuwa na imani na The One Whose Words Are The Final? Utararuliwa vipande vipande wala kaburi lako halitaonekana milele na milele. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni - Marekani wana demokrasia sana.
Hata South Wanayo Zuma Yuko Wapi ?!

Demokrasia Ya US Kwenye Kumchagua RAIS Ndio Napata Kigugumizi Naona wanatuhektia 2

Wananchi wanasumbuka 2 halaf kna kile kikundi cha wachache ndio kinamteua RAIS Kama sio wapuuzi wale wachache Huenda Leo US Ingekua Inaongozwa Namwanamama.....

... kweli kabisa yule mmama wa "some people did something" angekuwa anaongoza US.
 
Kwasababu ameshatoa kafara ya damu ya kasimu ikapelekea umwagikaji wa damu nyingine kwenye ndege ya Ukraine basi He is safe. Ni kutii masharti tu ya wafalme wa dunia ili aendelee kubaki madarakaini. Asingefanya hivyo...
 
Hata South Wanayo Zuma Yuko Wapi ?!

Demokrasia Ya US Kwenye Kumchagua RAIS Ndio Napata Kigugumizi Naona wanatuhektia 2

Wananchi wanasumbuka 2 halaf kna kile kikundi cha wachache ndio kinamteua RAIS Kama sio wapuuzi wale wachache Huenda Leo US Ingekua Inaongozwa Namwanamama.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina uhakika hiyo demokrasia ya uchaguzi wa US unayoilalamikia hujui ikoje, unalalamikia usichokijua!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
United States the most democratic country in the world! Ingekuwa kule kwingine sijui ungeanzaje au japo kuwa na wazo tu la "kutokuwa na imani" na His Holiness the Supreme Grand Leader? Yaani unaanzaje kuwaza kutokuwa na imani na The One Whose Words Are The Final? Utararuliwa vipande vipande wala kaburi lako halitaonekana milele na milele.
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom