Mashabiki Simba Bukoba, wamzawadia Ndemla fedha na mikungu ya ndizi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
MASHABIKI wa Simba wamemzawadia kiungo wa timu hiyo, Said Ndemla fedha na mikungu ya ndizi, baada ya kazi nzuri akiisaidia timu kushinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Ndemla alicheza vizuri jana na kufunga bao la kwanza, wakati bao la pili lilifungwa na Nahodha na mshambuliaji John Raphael Bocco, yote kipindi cha pili.

Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Ndemla aliwainua vitini mashabiki wa Simba SC dakika ya 69 kwa kufunga bao la kwanza akimalizia pasi ya kiungo wa pembeni, Shiza Kichuya.



Mashabiki wa Simba wakimzawadia kiungo Said Ndemla baada ya mechi jana Uwanja wa Kaitaba



Mpira uliozaa bao hilo ulitokana na makosa ya mshambuliaji wa Kagera Sugar, Atuepe Green aliyepiga bila uangalifu ukanaswa na Bocco aliyekimbia nao pembezoni mwa Uwanja kulia kabla ya kutia krosi iliyumkuta mshambuliaji Mganda Emmanuel Okiw aliyempasia kwa kichwa Kichuya ambaye naye alimpa Ndemla aliyefunga.

Baada ya hapo, Kagera Sugar waliokuwa wakicheza kwa kujihami kwa muda mrefu na kushambulia kwa kuvizia, wakaamua kufunguka moja kwa moja kusaka bao la kusawazisha.

Lakini hiyo nayo iliwagharimu kufungwa bao la pili kwa shambulizi la kujibiwa, beki Shomary Kapombe akimlamba chenga beki wa Kagera Sugar, Adeyoum Ahmed na kutia krosi nzuri iliyomaliziwa na Bocco kuipatia Simba bao la pili.

Ushindi huo unaifanya Simba SC irejee kileleni mwa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 14, ikifuatiwa na Azam FC pointi 30 na mabingwa watetezi, Yanga SC pointi 25.

Na baada ya mchezo mashabiki walimkimbilia Ndemla na kumpa zawadi mbalimbali kila mmoja kwa uwezo wake, wengine fedha, wengine mikungu ya ndizi.

Ikumbukwe Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameahidi kumnunulia gari Ndemla katika utaratibu wa kawaida aliojiwekea wa kuwazawadia gari wachezaji wanaojituma na wenye nidhamu kwenye timu.

Ndemla atakuwa mchezaji wa pili Simba kuzawadiwa gari na Poppe baada ya beki, Mohammed Hussein β€˜Tshabalala’ kupewa gari aina ya Toyota Raum Septemba mwaka 2016.

Na Hans Poppe amesema amevutiwa na Ndemla kutokana na nidhamu yake na kujituma bila kukata tama wakati wote.

β€œNi mchezaji ambaye hana neno anapokuwa hapangwi, na akiinuliwa kuingia uwanjani wakati wowote huenda kufanya vizuri na kuisaidia timu. Kwa kweli huyu kijana ni mfano wa kuigwa kwe wenzake na anastahili zawadi hii,”amesema.
Poppe amesema kwamba utamadunia wa kuwazawadia gari wachezaji wa klabu yake hiyo utaendelea na jukumu la kila mchezaji kuonyesha nidhamu na bidii kama Ndemla.

Chanzo: Bin Zubery Sports
 
Imekuganda na kukukera eeh. Mbona hizo fedha huulizi kuwa wameokota wapi? Kafuge Kambale bwawani pale
Sijaongelea pesa wewe angalia mkungu huo uko nusu na ndizi zimeanza kuharibika.
 
nadhani hata yeye hajui ATAUTUPA WAPI
Teh heheheheheeeee ahahahahaha hahhahahahah

We jamaa vipi, zawadi ni zawadi. Ila hilo la kuutupa wapi nalo neno, maana gharama ya kutupa siku hizi ni kubwa wakikukamata unatupa ovyo wanakugeuza mtaji
 
Teh heheheheheeeee ahahahahaha hahhahahahah

We jamaa vipi, zawadi ni zawadi. Ila hilo la kuutupa wapi nalo neno, maana gharama ya kutupa siku hizi ni kubwa wakikukamata unatupa ovyo wanakugeuza mtaji
nimewaza huo mkungu ulivyo toka Kagera hadi Dar KWA BASI heri awape wauza MTORI huko huko
 
Sijaongelea pesa we dada angalia mkungu huo uko nusu na ndizi zimeanza kuharibika.

Wasingeweza kubeba mkungu wote, hiko ni kwa ajili ya maonyesho, inasemekana ni canter kabisa limejaa mikungu ya ndizi.

Ni kama vile kwenye harusi mtu akipewa mifuko ya simenti, huwezi kuieleta ukumbini.

(natania lakini)
 
Ndio Tanzania pekee mchezaji anapewa helana mashabiki hadharani uku uongozi haukemei hii kitu.
Ndio mana wachezaji wetu hawawezi kwenda kupga soka nje ya nchi labda ajitambue
 
Ndio Tanzania pekee mchezaji anapewa helana mashabiki hadharani uku uongozi haukemei hii kitu.
Ndio mana wachezaji wetu hawawezi kwenda kupga soka nje ya nchi labda ajitambue
senti tu hizo
 
Wanaweza kukupa mikungu, changamoto ikawa kuisafirisha, ila ile nimeandika tu kukoleza kijiwe, sina uhakika nayo.
😑😑😑😑😑😑😑😑😑
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…