Mashabiki wa Arsenal FC mmemsikia Mtangazaji wa Choice fm Jimmy Kabwe?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kama ni ' Utani ' basi nadhani huu wa Jimmy Kabwe mtangazaji wa Choice fm umezidi na sina uhakika kama nikiweka hapa kile alichokisema leo katika Kipindi chake cha jioni ambacho hupenda kukitangaza kwa lugha yake anayoipenda ya Kiingereza akiwa na ' Mwanadada ' mmoja hivi Mrembo wana Arsenal waliopo hapa nchini Tanzania na hata huko kwingineko duniani watamuelewa.

Huku muda mwingi alipokuwa akitangaza leo Mtangazaji Jimmy Kabwe alisikika akiwa ' anainanga / anaisema ' vibaya Klabu ya Arsenal FC na wakati mwingine akiwa ' anaikejeli ' hadi kuifanya kama vile Klabu ya Arsenal haina ' hadhi ' yoyote ile duniani.

Ifuatayo ni nukuu ya Mtangazaji huyo wa Choice fm Jimmy Kabwe ambayo hata hivyo aliitoa tu ' Kiutani ' ila sijui wenyewe wenye ' litimu ' lenu la Arsenal mtaipokeaji ila Mimi kama Mimi GENTAMYCINE namuunga mkono huyu Mtangazaji kwa 100%.

" You know what supporting Arsenal FC is like dating a broke man " kwa tafsiri iliyotukuka kabisa ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili hapo Mtangazaji Jimmy Kabwe amesema kwamba " kuwa mshabiki wa Klabu ya Arsenal ni sawa na Mwanamke kuwa na Mpenzi asiye na Pesa / Mtonyo "

Hii ndiyo Liverpool FC bhana ' ukijipendekeza ' tu lazima upigwe nyingi sana na safari hii mtatukoma wana Anfield ambao siku zote kauli mbiu yetu inasema ' You will never walk alone ' na hakika kwa msimu huu Liverpool FC tutatembea ' ng'adu kwa ng'adu ' na zile timu zote kubwa zenye ' Kiherehere ' ambapo baada ya kumalizana na ' Wachovu ' Arsenal sasa tunawasubiri ' wabovu ' zaidi akina Manchester United, Chelsea, Manchester City, Tottenham Hotspurs na Everton.

Safi sana Jimmy Kabwe hilo ' dongo ' lako ulilowapa Arsenal FC leo ulipokuwa katika Kipindi chako Choice fm limeenda mahala pake.
 
Endelea kufanya assessment yako vizuri juu ya Timu bora msimu huu katika EPL,nakubali Liverpool this season mtatoa ushindani wa hali ya Juu kama misimu mwili au mitatu iliyopita lakini sioni kama mna pumzi ya kuchukua ndoo ya EPL.

Kwangu naipa nafasi kubwa sana Liverpool kuwa nyuma ya Man United itakapofika May.

Nimeangalia vikosi vyote viwili,makocha, ukubwa wa timu na mchezaji mmoja mmoja.

Kwenye makocha naona Mou anamzidi vitu vingi sana Kopp katika EPL, hasa uzoefu wake na mbinu.

Naisubiri kwa hamu game ya Liverpool vs Man United this season kuliko ya Man United vs Man City.

[HASHTAG]#GGMU[/HASHTAG] FC.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Dada Jane ! aka @GENTA kwa taarifa! ila tabia hizi za ushilawadu peleka mlima wa moto pale unapo kopa balimi au China bar unapo uzaga zegembe!
 
Hongereni ila mkikutana na Crystal Palace na Vibonde wengine vipigo ka kawa mnakaza game kubwa tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…