Mashabiki wa CR7 njooni hapa

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Ninamuelewa sana Ronaldo ndani ya uwanja kama CR7 ila Bado sijabahatika kumuelewa nje ya uwanja kabisa kama Baba wa watoto watatu.

Kinachonifanya nimuelewe ndicho kilicho kufanya na wewe uelewe akiwa na jezi nambari 7 mgongoni na kuipeleka mipira nyavuni.

Kinachonifanya nisimwelewe ni namna au njia anazotumia kupata watoto..... Mpaka sasa ana watoto watatu, Christian Jr au Christianinho na hawa Mapacha wa sasa hivi Eva na Matteo...... Tangu kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza Christian Ronaldo Jr mpaka Leo hajulikani Mama yake ila aliyehusika kubeba mimba sio Mama wa mtoto, yeye alilipwa tu kwaajili ya kubeba vitengeneza mimba vya wenzie (surrogate mother)...... Hawa Mapacha nao hali imekuwa vivyo hivyo Mama yao pia hajulikani baada ya Mama aliebeba mimba kujifungua na kulipwa fedha kwaajili ya kazi aliyopewa.

Situation hiyo ndiyo imeniacha na maswali mengi sana juu ya CR7 huyu huyu japo mpenzi wake wa sasa Georgina Rodriguez inasemekana ni mjamzito.

Wacha niendelee na research yangu labda ipo siku nitakuja kumwelewa kwanini anatumia wamama wa kukodi ili kubeba virutubisho vyao.... Christian vipi au haupigi kazi mzee ?.... Moja ya maswali ninayojiuliza kimya kimya.

Rafiki zangu madaktari najua kuna kitu mtaweza kuniweka sawa hapo kwa surrogate mother.


Nimeikuta sehemu hii
 
Kama technolojia hiyo isingekuwa na Gharama, naamini watanzania wengi wangeikimbilia...
 
Akistafu soka yake mengi yatajulikana ni swala la muda tu
 
Reactions: PNC
Huwezi kumwelewa, huyo sio Msabato. Ishi maisha yako. Usifuatilie maisha ya wengine. Ondoa Boriti ili uone vizuri kibanzi.
 
tena umkome huyo so dadako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…