Mashabiki wa Japan baada ya mpira kuisha wakusanya taka uwanjani na kuondoka

Walikusanya taka kwenye ile mechi ya kwanza ya Qatar na Ecuador video ikasambaa,ila nafikiria wangekua waAfrica wameokota wangetrend hivi? Au wangeonekana ni kazi yao,,,,Just saying!
Mwaka gani?
Kwani Qatar na Ecuador hawajakipiga bado
 

Hao jamaa ndio wanaongoza kwa ustaarabu na tabia nzuri duniani.

Na hapo hawamjui Yesu wala Allah wa Mtume muhammad.

Ila kina sisi wakristo na waislamu ibada nyingii ila tabia mbovuu
Mshaanza.


Huo utu, tabia njema na ustaarabu kuliko binaadamu wote walianza kuwa nao baada ya vita kuu ya pili au?
 
Hata ile michuano iliyofanyika kwao kipindi kile walifanya hivi hivi....
 
Hao jamaa ndio wanaongoza kwa ustaarabu na tabia nzuri duniani.

Na hapo hawamjui Yesu wala Allah wa Mtume muhammad.

Ila kina sisi wakristo na waislamu ibada nyingii ila tabia mbovuu
🤣🤣🤣🤣 Aise umemaliza kila kitu.👍
 
Nafahamu kuwa wana tabia nzuri

Jaribu ku imagine kama wangepigwa goli 7-0 huo usafi wangefanya?
Huenda wangefanya mkuu, sidhani kama wamefanya kwa sababu ya furaha. Bali ndivyo walivyo.
 
Kesho CCM wakiamka utasikia "tutakuwa kama Japan".

Haya mambo yanawezekana sehemu ambazo watu wana hulka zinazofanana. Sisi Nyerere alijaribu kutuunganisha ila wakati huo huo hata yeye kuna mizizi ya ubaguzi aliiweka na mpaka leo inatusumbua. Ubaguzi una athari kubwa sana za muda mrefu kwa anayebaguliwa, anayebagua na yule anayeshuhudia ubaguzi ukifanyika.

Hao wajapan kuna tamaduzi zao walitufundisha ilikuwa zianze kutumika katika uendeshaji wa Serikali ila baada ya juhudi zote mipango ikatupiliwa mbali.
 
Alihojiwa mmoja wa shabiki Mjapan akasema ni kawaida kusafisha baada ya kuchafua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…