Mashabiki wa Kaizer Chiefs ni mfano wa kuigwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ni baada ya kuingia uwanjani ili kuwatandika bakora wachezaji na makocha wa timu yao , baada ya kutolewa kwenye nusu fainali ya NEDBANK CUP baada ya kuchapwa na timu ya Free State leo hii

Tayari kocha wao Steve Komphela amejiuzulu nafasi yake .

Hili linatakiwa liwe fundisho kwa Timu ya Azam na mashabiki wake , haiwezekani timu kama Azam inayolipa wachezaji wake vizuri na imewapa kila kinachohitajika kwenye soka la kisasa kufungwa na Mbao au Stendi timu ambazo wachezaji wake hawajui hata watakapopata hela ya chai
 
Wachapweeeee tu...investment yote ile timu haina mafanikio ya aina tuliyotarajia
 
Nani kakwambia uwekezaji mkubwa ndio sababu ya kuchukua makombe, Leicester city alibeba ndoo mbele ya Manchester United,City,Chelsea,Liverpool na Arsenal team zenye mabilioni ya uwekezaji
 
Nani kakwambia uwekezaji mkubwa ndio sababu ya kuchukua makombe, Leicester city alibeba ndoo mbele ya Manchester United,City,Chelsea,Liverpool na Arsenal team zenye mabilioni ya uwekezaji
Hoja yako ni dhaifu sana .
 
Mpira ni zaidi ya uwekezaji.

Hujalazimishwa kuwa shabiki, kama unaona timu unayoshabikia haikupi unachotaka tafuta timu nyingine.
 
Wewe unashangaa hiyo cha mtoto huko ujerumani mashabiki wa timu ya humberg sv wameandamana mtaani na kuwaambia wachezaji wote kuwa timu ikishuka daraja wote watakula shaba na hadi sasa timu inaenda vizuri.Mashabiki wabishi wako ujerumani kawaulize Dotimund kilichowakuta.
 
me shabki sana wa tha amakhosi,,the galmour boys machief wenywe,,ila ktendo cha mashabiki its very stupid, ndio 2metoka nedbank cup sio 7bu ya kureact hvyo tho kiukwel hta lig hatubebi,sundowns wko njema zaid,ila ule upuuz unaweza leta maafa hta vifo mna wamuattack ad mlinz wa uwanjan pale,,sio ishu.. shabalala and others wako so disapointed,bodi ya ligi itatoa tamko na hatua soon..bye bye steve komphela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…