Mashabiki wa Lunyasi " ACHA TV TWENDE LUPASO"

Mashabiki wa Lunyasi " ACHA TV TWENDE LUPASO"

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wanasimbaaaaa!

Kwanza tukubaliane tuna game ngumu sana jumamosi hasa kutokana na historia ya timu za Morocco kuonea sana timu za Tanzania. Kuifunga Raja itakuwa historia mpya kwenye soka letu baada ya kuvunja uteja na timu za Egypt.

Ili tuongeze hamasa ni muhimu sana tuhamasishane kwenda uwanjani " ACHA TV TWENDE LUPASO". Hakika mashabiki kwa wingi wetu tutawapa nguvu ya kupambana vijana wetu.

Kingine ni kuvunja utamaduni wa kukata tamaa timu ikianza kufungwa au mpinzani akisawazisha! Uwanja unapoa, mitandao inachafuka! Sub akinyanyuliwa Kibu anazomewa!

Hii ni tabia chafu na inapaswa kukemewa! Akipewa nafasi Kibu tumshangilie kumtia moyo maana pale uwanjani hawakilishi mpinzani anafanya kazi yetu tumpe hamasa!

Tukubaliane wote "ACHA TV TWENDE LUPASO" na tushangilie vijana wetu hadi dakika ya mwisho hata kama tupo nyuma! Kama kuna lawama ni baada ya game! Timu imetimiza wajibu, mashabiki pia tumetimiza wajibu muda wote!

ACHA TV TWENDE LUPASO!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Tunaanza na Raja kwanza. huyu mgeni sijui tukampokee. Eti wanakuja lini?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wale wenyewe wanatosha, nasikia mashabiki wao lukuki wanaingia Dar toka jana.

Toleka bana Congo [emoji1787]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hata wakijaa uwanja mpaka Pomoni hawana impact yoyote.

Watanzania hatujui namna ya kushangilia, na hasa baada ya ujio wa mavuvuzela ndio ugoro, mtupu , kelele zisizo na mpangilio kama nyuki wapo kwenye mzinga.

Tukumbuke sauti za binafamu na matendo ambayo ni harmony ndio zinaweza kumtisha mpinzani.

❌ Dressing code huwa mbovu, Kila mtu anajivalia lisare la mwaka anaoujua mwenyewe au alo lokoteze kwenye mitumba zalo man u au asenal , ni Ningekuwa Mimi kama timu Ina rangi mbili basi Kila rangi ingekuwa upande wake ili kuleta tangu za kutosha.

❌ Kila katawi huwa kanakaa sehemu yake , na sare zake nyimbo zake na staili zake za kucheza. Hii hufanya uwanja kukosa umoja na hivyo kusababisha sauti zisizo na mpangilio. Yanayofanyika ulaya, Uarabuni na hata hapo mazembe Kongo twaweza kufanja.

❌ Hatuna nyimbo za hamasa za kuimba na halaiki tofauti sisi timu zote tunatumia wasanii wanaotunga nyimbo za singeli za kizaramo ambazo hazina mkong'osio wa halaiki na hivyo kukosa harmony.

Hizi ni baadhi ya nyimbo za mazembe za halaiki zenye mvumo na mkong'osio.
.

 
Hata wakijaa uwanja mpaka Pomoni hawana impact yoyote.

Watanzania hatujui namna ya kushangilia, na hasa baada ya ujio wa mavuvuzela ndio ugoro, mtupu , kelele zisizo na mpangilio kama nyuki wapo kwenye mzinga.

Tukumbuke sauti za binafamu na matendo ambayo ni harmony ndio zinaweza kumtisha mpinzani.

[emoji777] Dressing code huwa mbovu, Kila mtu anajivalia lisare la mwaka anaoujua mwenyewe au alo lokoteze kwenye mitumba zalo man u au asenal , ni Ningekuwa Mimi kama timu Ina rangi mbili basi Kila rangi ingekuwa upande wake ili kuleta tangu za kutosha.

[emoji777] Kila katawi huwa kanakaa sehemu yake , na sare zake nyimbo zake na staili zake za kucheza. Hii hufanya uwanja kukosa umoja na hivyo kusababisha sauti zisizo na mpangilio. Yanayofanyika ulaya, Uarabuni na hata hapo mazembe Kongo twaweza kufanja.

[emoji777] Hatuna nyimbo za hamasa za kuimba na halaiki tofauti sisi timu zote tunatumia wasanii wanaotunga nyimbo za singeli za kizaramo ambazo hazina mkong'osio wa halaiki na hivyo kukosa harmony.

Hizi ni baadhi ya nyimbo za mazembe za halaiki zenye mvumo na mkong'osio.
.

Ukweli mchungu! Tukifungwa tunakata tamaa na kuchanganyikiwa! Tunasubiri kanzu na chenga kushangilia. Lazima tuwe na mfumo wa kushangilia.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Madunduka FC mnaongoza kwa kutoka nje ya uwanja, mkifungwa tu.
Hamna vifua na imani na timu yenu.

Hamsa hamsa ikitembea hiyo Jumamosi, uwanja utabaki mweupee pee mtaniambia hapa...
 
Buku tatu mfukoni, chupa ya maji mkononi, tumboni ukiwa umeshiba ili kupata nguvu za kushangilia mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom