Mashabiki wa makala za wanyama mpo kwenye uzi upi jamani?

Mtafiti77

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,877
Reaction score
2,314
Habari nyote

Ninaomba kufahamishwa uzi makini unaojadili tabia za wanyama na maumbile ya dunia na vilivyomo hapa JF. Mimi ninapenda hizi mambo. Hunitoi National Geographic TV, Discovery channel...

Siku hizi nimenogewa na WildEarth Tv, hawa wanarusha video live toka mbugani kule South Africa. Ninatamani na sisi tungefanya hivi hapo Mikumi, Gombe, Serengeti n.k. Hawa SA vimbuga vimechoooka lakini wanavyojua kujitangaza mpaka inafurahisha. Dah! Kwa uzoefu wangu, hawaingii kwenye mbuga za kibongo hata kwa nusu kwa maana ya vilivyomo (uoto, wanyama, landascapes, n.k), sema wametuzidi hapo kwenye kujinadi tu.

Kwa sasa nipo nakula kitu live

https://www.facebook.com/
Ma-naturalists, ma-ecologists, ma-botanists, ma-zoologists n.k tafadhali tujuzane uzi huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…