Mashabiki wa Ronaldo na Messi msimu 2017/2018 mjiandae kisaklojia tuzo ya Ballon d’Or

Anayeongoza Kwa magoli Kwa Bara Zima la Ulaya ni MO SALAH mwenye magoli 41 mpaka Sasa Kwa mashindano yote Ronaldo wako ndio kwanza Ana 32 fuatilia records vizuri ndio uje hapa
Salah akichukua UEFA ndio anaweza sumbua kwenye hicho kinyang'anyiro. Ila vinginevyo vyovyote Mess na Ronaldo mmoja wapo atachukua.
 
Anayeongoza Kwa magoli Kwa Bara Zima la Ulaya ni MO SALAH mwenye magoli 41 mpaka Sasa Kwa mashindano yote Ronaldo wako ndio kwanza Ana 32 fuatilia records vizuri ndio uje hapa
La Liga Ronaldo ana magoli 24
Champions League magoli 15

Sasa hiyo 32 sijui umeitoa wapi mlinganishe na Salah na CR7 kwenye vitu vingine sio magoli
 
The only way Salah anaweza kuisogelea balon d'or ni kushinda UEFA!

hawezi kupewa balon d'or kama hana kombe lolote aliloshinda!

Lakini pia, kombe la dunia linaweza kubadili upepo. Yeyote atakaelishinda kati ya Messi na Ronaldo atachukua balon d'or.

Otherwise, nimemkubali Salah msimu huu. Ana kazi moja kubwa ya kuprove he is not a one season wonder!
 
Hii tuzo inaenda kwa kipa mwaka huu, Viongozi wa UEFA tushakaa tayari. Roma anabeba UEFA mwaka huu kwa masaada wa ALISON BECKER golini, alafu Brazil anabeba ndoo kwa kazi nzuri ya ALISON BECKER golini. Argentina group stage tu havuki. Portugal Robo fainali tu Mungu saidia.
 
Kwa miaka kumi mfululizo nilikuwa najua nani anachukua tuzo ya mwanasoka bora wa dunia kabla mshindi kutangazwa ila ya mwaka huu sijui nani atachukua kati ya cr7 au leo10
 
Ndugu ni timu mbili kwa sababu Liverpool na EGYPT national team zitaamua kama apewe au asipewe.
 
La Liga Ronaldo ana magoli 24
Champions League magoli 15

Sasa hiyo 32 sijui umeitoa wapi mlinganishe na Salah na CR7 kwenye vitu vingine sio magoli
LA liga 24
UCL. 15
Club world cup 2
Spanish super cup 1
Total 42
 
Kama Brazil atachukua world cup na neymar akashine basi neymar ndio mchezaji bora duniani sababu atakuwa na world cup,ligue 1 na FA ya ufaransa.
 
Kama Brazil atachukua world cup na neymar akashine basi neymar ndio mchezaji bora duniani sababu atakuwa na world cup,ligue 1 na FA ya ufaransa.
Neymar akiacha utoto uwanjani atazibeba hizi tuzo hadi achoke. Wenzie wakina Gaucho walikua hawaendi kwenye kibendela kila dk kumsubiri beki aje ampige chenga.
 
Ballon d'Or inapatikana kwa kura zinazopigwa na waandishi wa habari za michezo. Kura zinazingatia mambo mawili
1) Performance ya mchezaji uwanjani kwa mwaka uliopita
2) Nidhamu ya mchezaji hata nje ya uwanja kwa mwaka uliopita
Hii ina maana kwamba award ya mwaka 2018 itazingatia performance na nidhamu ya mchezaji kwa mwaka 2017/18

Mjumbe moja anawapigia kura wachezaji watatu
Chaguo la kwanza ina alama 5
Chaguo la pili ina alama 3 na
Chaguo la tatu ina alama 1

Makombe haya yanasaidia kupata point nyingi
  1. Kombe la ligi
  2. Kombe la mabara
  3. Kombe la klabu bingwa
Ndio maana kwa mfumo huu wachezaji kama akina Suarez ni vigumu sana kupata hii tuzo
Mohamed Salah anaweza kabisa kupata hizo point kama liverpool itawin UEFA na Egypt ikawin kombe la dunia hii ni lazima kwa sababu Liverpool imekosa kombe la ligi tayari. MO atapambana na akina Mesi, Neymar na wengineo ambao wao tayari wameshazichangia timu zao kushinda ligi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…