Mashabiki wa Simba SC wanadanganywa mchana kweupe. Wenyewe wanashangilia na kupongezana

Munch wa annabelletz47

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2019
Posts
1,885
Reaction score
3,227
- π—¨π—žπ—ͺπ—˜π—Ÿπ—œ π— π—–π—›π—¨π—‘π—šπ—¨.

Klabu ya Simba inaongozwa Kwa Propaganda hapo awali ilipokuwa inaingia mkataba na M-Bet, Simba hawakuweka bayana kuwa huo mkataba unathamani ya kiasi gani,

Yanga SC walipoingia Mkataba Mpya na SportPesa na walisema mkataba huo unathamani ya Billion 12. Baada ya siku Simba wakaja na drama ya kusema mkataba wao na M-Bet ni Billion 26 kama sikosei.

Na hizo Billion 26 zilikuwa hazijaandikwa kwenye hundi bali ziliandikwa kwenye jezi.

Mkutano Mkuu wa Simba SC wa msimu walisema kuwa bajeti kuu ya Msimu ujao 2023/24 ni Billion 13 ikawaimepita hiyo. Juzi Klabu ya Yanga imefanya Mkutano Mkuu na kusema kuwa Bajeti kuu ya Msimu ujao 2023/24 ni Billion 20.

Baada ya siku 1 CEO wa Simba SC Imani Kajula amesimama mbele ya umma anasema Bajeti kuu ya Simba SC msimu huu ni Billion 24 ambapo Kuna Billion 11 zimeongezeka.

Kiufupi Klabu ya Simba SC inaongozwa Kwa Propaganda na hawataki wao wazidiwe na Yanga SC!! Ndio maana Kila siku drama haziishi.
 
Yanga princess na Lucy aymel mmeshamlipa pesa zake nyie utopolo au mnajisahaulisha
 
Hao ni mbumbumbu ila huwa nasemaga humu nyie watanzania mna ujinga ujinga mwingi ndio maana mko mnadanganywa kila siku
 
Sema umepigwa na kitu kizito baada ya kuona bajeti ya Simba imeongezeka! Simba inaenda kushiriki michuano ya Super League ambayo hadi mkutano unafanyika mwaka jana, michuano haikuwapo wala chanzo cha fedha hakikuwapo. Sasa CAF watatoa sh. 5.8B za maandalizi tu, narudia, za maandalizi tu!
Mahitaji mapya, Mapato mapya, Bajeti mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…