May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kwanza niweke rekodi sawa. Tanzania hakuna Wapenzi wengi wa Mpira wa Miguu kama wanavyoamini wengi wetu, bali kuna Mashabiki wengi wa Simba na wa Yanga.
Kwa isivyo bahati mashabiki wetu hawa wanachowazidi Mashabiki wa sehemu nyingine Duniani ni namna hata wanavyoshabikia hizi timu zao.
Leo hii Yanga au Simba wakipoteza mchezo au kushinda basi Mashabiki hapo hapo hugeuka Washauri, Wachambuzi, Wakosoaji, Wataalamu wa soka, Mahakimu n.k.
Wakati alipoondoka Kocha wa Simba mwishoni wa msimu uliopita timu ilikuwa chini ya Matola, na walipopata matokeo mazuri kwnye mechi zilizobakia kila Mtu aliimba na kutaka Matola akabidhiwe timu....lakini kwa sasa miezi takriban mitano baadae ni Mashabiki hao hao sasa wanataka Matola aondoke.
Hali ni hivyo hivyo kwa Wachezaji, juzi wanasema Mzungu tumepigwa, leo Mzungu anajua....kesho tena akiamka vibaya watamgeuka kusema tumepigwa.
Na sasa kumeanza wimbo wa kutaka Mgunda apewe timu, kisa tu kahinda mechi zote alizosimamia mpaka sasa, sasa ngoja apoteze uone atakavyoshambuliwa kama hawamjui.
Kwa maoni yangu Simba waendelee na mchakato wa kumpata Kocha na Mgunda na Matola waendelee kuwepo benchi la ufundi, au timu ya vijana n.k.
Kama ni kuachiwa timu basi iwe ni mbeleni huko, kamwe tusiendeshwe na Mashabiki hawa wasio na subira hata kidogo....ingawa hii haimaanishi kuwa siutambui mchango wa Mashabiki.