Mashabiki wa timu ya Mashujaa FC wameanza kuliteka Vibe la Soka la Tanzania

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Mashabiki wa timu ya Mashujaa FC wameanza kuliteka Vibe la Soka la Tanzania ambalo limeanza kupoteza mvuto wake kwa timu za mikoani. Ukiachana na Timu za Simba na Yanga pamoja na Azam kwa kiasi chake timu nyingine ambazo ziliteka hisia za mashabiki kiasi cha kufanya biashara ya Jezi zao Tanzania walikuwa ni Mbeya City ambao walizungumzwa kila kona ya Tanzania na kila shabiki wa Mpira Tanzania hasa kutokea mikoa ya Nyanda za Juu Kusini alijisikia Fahari kuivaa Jezi ya purple ya Mbeya City na ilikuwa na mvuto wake.

Wakiwa kwenye Kilele cha mafanikio ya kufanya vizuri upande wa Mashabiki iliibuka timu ya Stendi United ya Shinyanga ambayo ilikuja kuivuruga Mbeya City na hapo tukajua imekwisha. Hatimaye walikuja Singida United ambao nao walijaribu kuteka hisia za mashabiki wa soka lakini walipotea na hatujui nini kiliwakuta.

Na sasa Zama mpya zimeiibua Timu ya Mashujaa FC ya mkoani Kigoma ambayo Vibe la mashabiki wake linakwenda kufunika zama zile za Mbeya City, Stendi United na Singida United.
Tutarajie makubwa kutoka kwa Mashabiki hawa waliolewa Soka la Timu yao ambayo ni alama ya Mkoa wao.

#solomatv_updates

MASHUJAA NA ZAMA MPYA ZA BOLI LA BONGO
 
Shida wa mpira wetu Hawa watapigwa misumari na tff na wadau wa soka mpaka wakubali shoo

Ligi yetu watu Wanataka ibaki kua Simba na Yanga tu ndo maana hatuendelei

Azam wenyewe na mapesa Yao wanaijua shoo
 
Wakianza tu kupokea vipigo mfululizo, pumzi itakata mapema sana. Ni suala tu la muda.
 
Bado hawajashudia kipigo kwa timu yao wakiwa wengi hivyo, subiria kwanza wapigwe mechi 3 mfululizo kama watabaki hivyo hivyo ndio uandike hayo uliyo andika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…