Mashabiki wa Yanga nani kawaroga?

Mashabiki wa Yanga nani kawaroga?

wajibisha

Member
Joined
May 16, 2021
Posts
90
Reaction score
215
Simba imezindua jezi kuelekea msimu mpya. Tuseme basi jezi za Yanga ni bora zaidi ya Simba. Halafu?

Kwa miaka kadhaa Yanga wamekua wakijanasibu kuwa na jezi bora. Sasa tujiulize maswali, mbona matokeo ya uwanjani ni tofauti?

Achana na hiyo, Simba anavuta Tzs 1 Bilioni kwa Mwaka kutoka kwa Vunja Bei bila kujalisha zitauzwa ama hazitauzwa. Smart Brain.

Sasa tuwaulize Yanga, wanapata mgao wa kiasi gani kutoka GSM kila mwaka. Hakuna atakayedhubutu kuuliza. Ni ujanja ujanja tu.

Badala ya mashabiki wa Yanga kushughulika na jezi za Simba, wawaulize viongozi wao wamepokea kiasi gani mwaka jana kwenye mauzo ya jezi. Ni aibu hata kutaja.
 
Ngoja nibanze hapa pembeni nishuhudie huu mpambano
 
Nawasilisha..
Screenshot_20210903-150408.jpg
 
Badala ya mashabiki wa Yanga kushughulika na jezi za Simba, wawaulize viongozi wao wamepokea kiasi gani mwaka jana kwenye mauzo ya jezi. Ni Aibu hata kutaja.
Mkuu acha mashabiki wenzetu wa Simba akina GSM na Sandalendi wazivune hela za mashabiki wa utopolo, maana kuna wengine wameuziwa hadi sh. 100,000/= jezi moja, katika hizo uto wanapata sh. 1,300/=
 
Mtatusamehe wanasimba kwa kuongeza tarehe ya kuzaliwa kwa Boss kwenye jezi MO29
hiyo MO29 ni sabuni ya kuondoa nuksi mikosi ya kutobeba kombe
pia inaondoa misukule kwenye jezi za uto

FB_IMG_1630672856856.jpg
 
Mmh mashabiki wa simba huwa wepesi kupanic.

Mbona nyie mmewasema yanga wee,jezi yao mmiedit mtakavyo hadi kuifananisha na limao

Zamu yenu imefika mapovu tele aiseee
Hao hawana ustahimilivu kabisa,hata kipindi kile cha Manara anatusimanga tulivulimia lakini wao sasa hivi kibao kimegeuka wanakaribia kurusha ngumi.
 
Mtatusamehe wanasimba kwa kuongeza tarehe ya kuzaliwa kwa Boss kwenye jezi MO29

Leo unaranda randa na Comment hii kila mahari.Pata Mo Energy Mtani ikuongezee nguvu,maana naona kabisa unakoelekea leo si kuzuri [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wanajitapa wana kila kitu ila bado hawajaridhika yaani kuna kitu wanaona yanga wanacho ila wao hawana. Makombe wanabeba ya kutosha,wana boss wanayemtetea kila kukicha,wana CEO mrembo ila bado wanaona wamepungukiwa pakubwa,maisha ya mateso sana

Manara katusimanga mno,marrison wamemchukua kibabe bado tu daah ingekua ni wao pasingekalika
Hao hawana ustahimilivu kabisa,hata kipindi kile cha Manara anatusimanga tulivulimia lakini wao sasa hivi kibao kimegeuka wanakaribia kurusha ngumi.
 
Back
Top Bottom