Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kilele ya Wiki ya Mwananchi Agosti 4, 2024 kutakuwa na tuzo maalumu iliyoandaliwa na mashabiki wa timu hiyo kwa ajili ya kumkabidhi kiungo Khalid Aucho.Mashabiki hao wamemwandalia tuzo hiyo baada ya kumchagua kuwa mchezaji bora baada ya kukosa tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) misimu miwili mfululizo.