Dong Jin
JF-Expert Member
- Jun 4, 2018
- 968
- 2,034
Jana baada ya mechi ya Yanga Vs Tabora kumalizika, licha ya timu ya yanga kupoteza mara ya pili mfululizo kwa bao 3-1 tena wakiwa uwanja wa nyumbani, mashabiki wa yanga karibia asilimia 80 walisimama na kuwapigia makofi wachezaji wao kuwapongeza kwa kazi kubwa waliyoifanya.
Hii ni maturity ya hali ya juu sana katika mpira wetu hasa pale hizi timu mbili za mizimu ya nchi zinapofungwa na mashabiki wakaungana na wachezaji wao kuwapongeza kwa kazi nzuri
Yawezekana wameanza kulielewa soka la dunia linavyoenda kuwa kila timu lazima ipitie kipindi kibaya hasa pale inapokuwa imepata mafanikio makubwa msimu wa nyuma yake pamoja na kuwapoteza key players wake. Safu ya ulinzi ya yanga imekumbwa na majeraha pamoja na kadi kiasi cha kumlazimu mwalimu Gamondi awatumie viungo wakabaji na mawinga km mabeki (Aucho, Andambwile na Nkane) jambo linalofanya wapitike kiurahisi kwa kuwa hawana uzoefu wa kutosha kucheza km mabeki
Hiki kitu ndo kinachowakumba hata man city msimu huu wamefungwa mechi nne mfululizo!