Mashabiki ya Yanga sc hawautaki tena uwanja wa Azam complex- Chamazi! Wataka mechi zao zikachezwe KMC complex stadium

Mashabiki ya Yanga sc hawautaki tena uwanja wa Azam complex- Chamazi! Wataka mechi zao zikachezwe KMC complex stadium

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,359
Reaction score
6,568
Lilikuwa suala la muda tu baada ya Bundi mzee kuwika katika uwanja wa Chamazi, klabu namba moja kwa masuala ya ushirikina Tanzania.

Daima mbele nyuma mwiko kuanza harakati za kuukimbia uwanja wao wa nyumbani ,Chamazi na kutaka kuja kuutumia uwanja wa KMC unaotumiwa na mahasimu wao wanaoongoza katika msimamo wa ligi kuu ya NBC- Tanzania, naizungumzia Simba Sc.

Je, kufungwa na Azam na Tabora United ndio kunawafanya muukimbie uwanja au kuna sababu nyingine za kishirikina?
 
Mpira wa Bongo bhana 😂 hao Yanga c walikuwa wanawacheka simba walivyoukataa uwanja wa chamazi baada ya kulambwa sasa na wao baada ya kubanduliwa ety hawautaki 😂 mbona wakishinda hawasemi hawataki uwanja kisa wameshinda
 
Maamuzi haya ni sura na akili halisi za Mwafrika.
 
Ukiona vijisababu vinakua vingi ndio kupoteana kwenyewe...Hawa msimu watakukuruka Sana lakini watafeli . Huko CL kuna kila dalili hawatoboi
 
Tate Mkuu aende akawafariji
Mashabiki wa Yanga tuko poa tu. Na hata hiyo timu ifungwe magoli 20! Bado tutaendelea tu na maisha yetu ya kila siku.

Binafsi siwezi kupata changamoto ya kiafya, kwa sababu tu Yanga imefungwa! Nadhani kuna mambo mengi ya msingi yanatakiwa kuniumiza kichwa. Ila siyo haya mambo ya mpira.
 
Mpira ni mchezo wa bahati na kukataa uwanja usio na bahati nasi wana utopolo ni sawa, Azam tuhameeee!! Wameroga uwanja tufungwe!! Hata Baka hakujielewa kama anadaka mtu!!! Tangu Baka katoka timu imepoteana pale nyuma, bado hatujaziba pengo lake na Tabora United wakastudy na kupata mwanya basi sio kujisifu huko kumbe wametumia pengo la Baka tu.

My take
Yanga imefungwa magoli manne kwenye ligi hadi sasa, magoli yote tuliyofungwa yametokea katikati sehemu ya juu kidogo ya box wanapocheza Job na Baka, hapo ndo panavuja hawa miamba wanapokosekana, tatizo dogo tu Gamondi atafute mwarobaini. Yanga bingwa.
 
Bado hujasema
 
Back
Top Bottom