Mpira ni mchezo wa bahati na kukataa uwanja usio na bahati nasi wana utopolo ni sawa, Azam tuhameeee!! Wameroga uwanja tufungwe!! Hata Baka hakujielewa kama anadaka mtu!!! Tangu Baka katoka timu imepoteana pale nyuma, bado hatujaziba pengo lake na Tabora United wakastudy na kupata mwanya basi sio kujisifu huko kumbe wametumia pengo la Baka tu.
My take
Yanga imefungwa magoli manne kwenye ligi hadi sasa, magoli yote tuliyofungwa yametokea katikati sehemu ya juu kidogo ya box wanapocheza Job na Baka, hapo ndo panavuja hawa miamba wanapokosekana, tatizo dogo tu Gamondi atafute mwarobaini. Yanga bingwa.