Mashabiki Yanga wampiga ngumi shabiki wa Simba

martial jb

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
863
Reaction score
1,462
Habari wakuu,

Katika hali inayoonekana si ya kawaida, shabiki mmoja wa Simba ameambulia kichapo kutoka kwa mashabiki wawili wa Yanga jana mnamo saa 2 usiku, pale Keko(Temeke, Dar Es Salaam).

Mashabiki hao awali inasemeka walikuwa wakibishana kawaida tu, ila shabiki wa Simba alionekana kuwatania sana Yanga huku akiwaita majina yanayokera na kuudhi mashabiki hao wa Yanga.

Baada ya muda inasemekana wana Yanga hao uvumilivu uliwashinda ndipo mmoja kati yao alipotoa lugha ya kuonya kurusha ngumi endapo mwana Simba huyo ataendelea na utani. Jambo ambalo lilitimia baada ya shabiki huyo kumpiga ngumi kijana huyo iliyompeleka chini, na ndipo wote wawili hao walionekana kumchangia kwa kumpiga kwa hasira mwana Simba huyo na kutokomea.

Mpaka watu wa pembeni wanaenda kutetea ugomvi huo, tayari yule shabiki alishachakazwa vibaya huku wana Yanga hao wakionekana kukimbia mbio mbali na eneo hilo.

ANGALIZO: Mashabiki kuweni makini na utani wenu, isifikie hatua kama hiyo inayotaka kufikia kwakweli.

Pia kuweni makini na wana Yanga, maana kwa sasa ni kweli wana msongo wa mawazo na wamechanganyikiwa na hali halisi, MSIWATANIE SANA maana siyo vizuri na ni hatari.

Pia mashabiki wa Yanga, jaribuni kuwa na busara za kimichezo, jambo kama hili ni la kipuuzi, hata kama una hasira.
 
Washabiki wa mpira hasa Simba na Yanga ni watu wenye matatizo ya akili. Wakianza kubishana lazima watengeneze uhasama na wana tabia ya kuchokozana kila mara.

Matatizo makuu ya Watanzania ni kushabikia Simba, Yanga na Vyama vya siasa.
 
Washabiki wa mpira hasa Simba na Yanga ni watu wenye matatizo ya akili. Wakianza kubishana lazima watengeneze uhasama na wana tabia ya kuchokozana kila mara.

Matatizo makuu ya Watanzania ni kushabikia Simba, Yanga na Vyama vya siasa.
Kuwa na ushabiki sio mbaya,
Ila hatua au aina yao ya ushabiki naona imefikia pabaya
 
DAWA YA MOTO NI MOTO,DAWA YAMZOZO KIPIGO.
 
Ndio ukaamua ufungue na uzi hapa JF,? Mnashusha hadhi ya jukwaa kwa kuweka nyuzi za kipuuzi! Bila shaka wewe ni shabiki la utopoloni ndio uwa mna akili za kupima kwenye kibaba.
Yaani jamaa anaweza hata kutuletea story za kunyimwa chakula, na shemeji yake mtata humu jukwaani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…