Mashabiki Yanga waomba MO afadhili Yanga

martial jb

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
863
Reaction score
1,462
Habari wakuu

Katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya mashabiki wa Yanga wanasemekana kwenda office za kampuni ya Metl (Mo enterprises Ltd) zilizopo Posta Dar es Salaam. Mashabiki hao wanaotokea baadhi ya matawi ya yanga, wanasemekana kuandika barua inayoomba ufadhili wa timu yao kutoka kwa bilionea Mohammed Dewji, huku wakionesha msimamo mkali katika kuukataa ufadhili wao wa awali (GSM).

Mmoja wa walinzi wa ofisi hizo aliyekataa kutaja jina lake ameeleza kuwa, kundi la mashabiki hao wamekuwa wakishinda ofisini hapo kutaka kuonana na tajiri huyo huku wakikosa nafasi hiyo.

Je, Mo dewji anaweza kukubali ombi hilo hali ya kuwa hana mapenzi na klabu hiyo. Na je, wana Simba na wana Yanga watalichukulia vipi suala hili, ndiyo maswali yanayokuja moja kwa moja kichwani.

Lakini ngoja tuone itakavyokuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…