BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mashahidi 10 na vielelezo nane vinatarajia kutolewa katika kesi ya kukata nyaya za umeme katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo jijini Dar es Salaam na kusababisha hasara ya Sh316 milioni, inayowakabili wafanyabiashara watatu wakazi wa Mbagala na Tandika.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Erick Rushenzirana (20), Baruani Baruani (39) na Emmanuel Darosh, ambao wanadaiwa kuingilia miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kukata nyanya za umeme na hivyo kulisabishia hasara shirika hilo, kinyume cha sheria.
Mashahidi hao wanatarajia kuanza kutoa ushahidi Januari 10, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika na washtakiwa kusomewa hoja za awali (PH).
Leo Jumatano Desemba 28, 2022 wakili wa Serikali Caroline Matemu, amedai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kwamba anaomba kuwamsomea hoja za awali washtakiwa hao.
Baada ya kueleza hayo, wakili Matemu aliwakumbusha mashtaka washtakiwa na kisha kuwasomea hoja za awali (PH), mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mery Mrio.
Akiwasomea hoja za awali, Matemu amedai kuwa Januari 14, 2022 katika Soko Kuu la Kariakoo, washtakiwa kwa pamoja waliharibu kebo zilizokuwa zikienda kwenye mtambo mkubwa umeme na hivyo kulisababishia Shirika la Umeme nchini( Tanesco) hasara ya Sh 316,980,333.78.
Amedai siku hiyo ya tukio, majira ya alfajiri katika eneo hilo, washtakiwa walikamatwa na walinzi katika geti namba tano na walipopekuliwa walikutwa na misumeno miwili, spana nane, vichwa vitano vya spana, bisibisi nne, kipande cha minyororo, wembe mmoja wa randa, Praizi na kipande kimoja cha kebo ambavyo vilikuwa ndani ya kibegi chenye rangi nyekundu.
Pia wanadaiwa kukutwa na nyaya za umeme walizokuwa wameweka katika ndoo ya rangi ya njano.
Washtakiwa baada ya kukamatwa na walinzi wa soko hilo, waliwachukua wote na kuwasilisha kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kuandikwa maelezo yao.
Wakiwa kituoni hapo, hati ya kuhifadhi mali iliandaliwa na vitu hivyo vilihifadhiwa na askari polisi mwenye namba E 7130 Sajenti Nowa mbele ya shahidi, Shabani Mwenda.
Hata hivyo, Soko la Kariakoo lilifanyiwa ukaguzi na kubainika kuwepo uharibifu katika mfumo wa umeme na baada ya kufanyika tathmini na Mamlaka husika ilibainika kupatikana na hasara ya Sh316, 980,333.78.
Baada ya upelelezi wa awali kukamilika, washtakiwa walifikishwa Mahakamani hapo kujibu tuhuma zinazowakabili.
Washitakiwa baada ya kusomewa maelezo ya shtaka linalowakabili waliyakana isipokuwa kukamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Msimbazi.
Wakili Matemu baada ya kueleza hayo, hakimu Mrio amesema kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa ushahidi wa upande wa mashtaka Januari 10, 2023 hivyo upande wa mashtaka siku hiyo wapeleke mashahidi wa kutosha.
MWANANCHI