JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Maelezo ya mashahidi hao 52 yamesemwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Elipokea Yona na mwendesha mashitaka wa mkoa wa kagera Waziri Magumbo pamoja na mawakili wengine wa serikali ambao ni Nassoro Katuga, Sabina Silayo, Erick Mabagala pamoja na Matrida Assey.
Kwa mujibu maelezo ya mashahidi 52 yaliyosomwa na mawakili wa serikali Mahakama hapo yamebainisha kuwa mshitakiwa namba moja ambaye ni padri Elipidius Rwegoshora alikili wakati alipohojiwa kuwa ndiye aliyepanga njama za kufanya utekaji na kufanya mauaji ya mtoto Noela Asimwe Novath kwa kumshawishi mshitakiwa namba 2 Novath Venant ambaye ni Baba wa mtoto huyo na kumuahidi iwapo atafanikiwa kupata baadhi ya viungo vya mtoto huyo atampa fedha za kitanzania milion 30, kumnunulia Gari nyeusi aina ya V-8 pamoja na kumwezesha kwenda kuishi katika jiji la Dar es Salaam yeye na mke wake.
Maelezo mengine ni kuwa washtakiwa baada ya kufanikiwa kumteka na kumuuwa mtoto Asimwe mshitakiwa namba moja ambaye ni padri Elipidius Rwegoshora aliwaambia washitakiwa wengine akiwemo Baba mzazi wa mtoto Asimwe kununua sumu ya panya na kukaa nayo mda wote ili wakikamatwa na polisi wanye sumu hiyo wafe ili wapoteze ushahidi na kuwaambia kuwa wao baada ya kufa angetunza familia zao ambapo katika Maelezo yaliyosomwa Mahakama hapo.
Chanzo: Global TV
~ Watuhumiwa 9 wa mauaji ya Asimwe wadai hawajui kosa lao
~ Kagera: Watuhumiwa tisa wa mauaji ya Asimwe Novart wafikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la kuua kwa kukusudia
~ Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji