Mashairi (Lyrics) ya wimbo wa Sisi Ni Wale wa Phina

Mashairi (Lyrics) ya wimbo wa Sisi Ni Wale wa Phina

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Msanii wa Bongo Fleva, Sarah Michael Kitinga "Phina" aliimba ujumbe huu kupitia Wimbo wa "Sisi Ni Wale" aliouweka kwenye Chaneli yake ya YouTube, Desemba 29, 2023 na hadi Novemba 28, 2024 umetazamwa zaidi ya mara Milioni 10.99.

Wimbo ulilenga zaidi kumpa Mtu Moyo wa kuendelea kujituma katika Maisha hata kama kuna wakati mambo hayaendi vizuri

SISI NI WALE
Chorus:-
Sisi ni wale tuliosaidiwa na Mungu
Sisi ndo wale tuliobarikiwa na baba
Sisi ni wale tuliosaidiwa , ah na Mungu
Sisi ndo wale tuliobarikiwa na baba

Verse 1
Sina hela, sina pesa ,sina doh
Sina nyumba, sina gari, sina ooh
Kila kukikucha mi naiwaza kesho
Napiga moyo konde nitafika ooh
Wanaokudharau leo,
watakusalimiea kesho
(Kwa heshima)
Wanaokusema sema,
watakusifia kesho
Unaokula nao
Na kucheka nao (oh)
Kesho ukidondoka
Hutokuwa nao
Piga moyo konde
Wakati wa Mungu
Wakati sahihi hihi
Piga moyo konde
Wakati wa baba
Wakati sahihi hi hi

Chorus:-
(Sisi ni wale)
Sisi ni wale tuliosaidiwa na Mungu
Sisi ndo wale tuliobarikiwa na baba
Sisi ni wale tuliosaidiwa , ah na Mungu
Sisi ndo wale tuliobarikiwa na baba

Verse 2
Jana niliumwa
Nikadhani nitakufa
Leo niko fiti ukinicheki
Nadundika
Nilipoachishwa kazi
Walidhani nitasota
Leo nipo juu ile kibosi
Nadundika

Kama unaamini
Umesaidiwa na Mungu
Piga kelele, kelele moja (eh)
Kelele mbili (eh, eh)
(Eh, eh)
Kama unaaminiu Umesaidiwa na Mungu eeh
Piga kelele, kelele moja (eh)
Kelele mbili (eh, eh)
(Eh, eh)

Chorus:-
Sisi ni wale tuliosaidiwa na Mungu
Sisi ndo wale tuliobarikiwa na baba
Sisi ni wale tuliosaidiwa , ah na Mungu
Sisi ndo wale tuliobarikiwa na baba
 
Back
Top Bottom