1.
Leo inanigharimu,kuleta kwenu andishi,
Lahusu Kesi adhimu, Bodi ya CUF kughushi,
Msome wote Kaumu, Jaji yake matamshi ,
Bodi ya Lipumba ghushi, imehukumu hukumu,
2.
Kwa mujibu wa hukumu, kufutwa sababu ghushi,
Bodi Lipumba haramu, si BODI bali uzushi,
Kunyang'anywa majukumu, tumemaliza Ubishi,
Bodi ya Lipumba ghushi, imehukumu hukumu
3.
Jaji yake maelezo, baada ya linganishi,
Bodi haina Vigezo, pungufu vidhibitishi,
Ipo nje ya mwongozo, wa vigezo halalishi,

4.
Jaji katika mafunzo, kaleta na patanishi,
Bodi halali ya mwanzo, hile Bodi anzilishi,
Hukumu ya hadhi tunzo, tufurahi ni ucheshi,

5.
Hukumu hii salamu, fununu ya Moto Moshi,
Marofa wa ufahamu, watumwao Watumishi,
Dhalimu hujidhulumu, nafusi zao kwa zushi,

6.
WANAFIKI madhalimu, daima hadhi tapishi,
Si Binadamu timamu ,Bongo lala ni wabishi,
Yajayo kwao msimu, wa kubeba mafurushi,

7.
Yajayo ya tabasamu, furaha kisababishi,
Siku hiyo ni muhimu, Buguruni hapatoshi,
Inshaallah haki tatimu, litatoka hatarishi,
Bodi ya Lipumba ghushi, imehukumu hukumu.
Na mwandishi wetu mtaalam wa lugha ya Kiswahili.