Mashamba ya wazungu Afrika Kusini sasa staili ya Zimbabwe

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
pic+mashamba.gif

Wabunge 241 wa Afrika Kusini wameukubali na wengine 81 kuupinga muswada wa kutaka kutwaliwa na kununuliwa ardhi kwa nguvu katika nchi hiyo.

Hadi Agosti 30 mwaka huu, Kamati ya Bunge la nchi hiyo imetakiwa ichunguze kama mabadiliko ya Katiba yanawezekana ili Serikali iweze kutwaa ardhi za watu binafsi.

Muswada huo hapo kabla uliwasilishwa na chama cha mrengo mkali wa shoto, Wapiganaji wa Ukombozi wa Kiuchumi (EFF).

“Wakati wa maridhiano umepita. Sasa umefika wakati wa kutolewa haki,” alisema kiongozi wa EFF, Julius Malema.

Aliwaelezea wakoloni wa zamani wa Kiholanzi huko Afrika Kusini kuwa ni “wahalifu waliotunyang’anya ardhi yetu”.

Alisema wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi, vizazi vyao viliwatenga na kuwabakisha Waafrika katika makambi ya vizuizi ambayo leo yanaitwa mitaa ya Waafrika.

Muswada huo pia umeungwa mkono kwa wingi na wabunge wa Chama Tawala cha ANC. Katika mkutano wake mkuu Desemba mwaka jana, chama hicho kilitangaza msimamo mkali kuhusu suala la kugawa ardhi. Kwa vile kuna uchaguzi mkuu mwakani, chama hicho kinajikuta hivi sasa katika mbinyo. Na ilivyokuwa sasa kimeukubali muswada huo inawezekana kikaungwa mkono na wapiga kura wengi zaidi miongoni mwa raia wa Kiafrika walio maskini.

Mbunge Thandeka Mbabama aliuelezea uamuzi huo kuwa ni mbinu ya kubadilisha dira, kujaribu kuyafumbia macho makosa yaliyofanywa hapo kabla na ANC.

Rushwa na ufisadi pamoja na kushindwa kuwapatia wakulima wa Kiafrika mafunzo na vifaa ndio kizingiti kikubwa cha kuleta marekebisho ya ardhi yaliyoahidiwa na chama hicho katika ilani zake za uchaguzi za hapo kabla.

Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Afrika Kusini umegundua kwamba robo tatu ya ardhi ya kilimo iko mikononi mwa wakulima wa Kizungu, si kidogo kama walivyokuwa nayo mwishoni mwa utawala wa kibaguzi. Wakati huo walishikilia asilimia 85. Lakini bado haijulikani lini Bunge litajadiliana juu ya mabadiliko haya ya katiba.

Shauri hilo la kutwaa mashamba, na ikilazimika bila kulipa fidia inayostahiki, limepingwa na wakulima.

Rais wa Shirikisho la jumuiya za wakulima wa Afrika Kusini, Agri SA, Dan Kriek amesema hatua hiyo haiingii akilini, kwani inaumiza uchumi wa mabenki ambayo yamewekeza sana katika kilimo. Alisema hoja kama hizo za kimsingi hazijatiliwa sana maanani katika mdahalo, na pia ni kwamba wazungu na Waafrika wote wana haki ya kumiliki mali katika nchi hiyo.

Suala la kutaka kutwaliwa ardhi limekuwa tete katika Afrika Kusini tangu kumalizika kipindi cha ubaguzi. Katika hotuba yake ya kwanza tangu alipokamata urais wa nchi hapo Februari mwaka huu, Cyril Ramaphosa aliunga mkono kutwaliwa mashamba hata bila ya kulipwa fidia, ila tu uzalishaji wa mazao ya kilimo, hasa yale ya vyakula, upande. Aliahidi kwamba ataharakisha Waafrika wanagawiwa ardhi.

Sababu kubwa ya kuchukuliwa hatua hii hivi sasa ni kwamba, licha ya kupita miaka 24 tangu kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi katika Afrika Kusini, bado sehemu kubwa ya ardhi ya kilimo katika nchi hiyo imo mikononi mwa wakulima wa Kizungu.

Kuna utafiti mwingine ulioonyesha kwamba licha ya wazungu wa Afrika Kusini kuwa ni asilimia tisa tu ya wakazi, lakini wao wanamiliki asilimia 73 ya ardhi inayotumiwa kwa kilimo.

Hata hivyo, wahakiki wanahofia kwamba uamuzi huu wa Afrika Kusini katika siasa yake ya maendeleo unaweza ukaielekeza nchi hiyo katika ile njia iliyofuatwa na nchi jirani ya Zimbabwe chini ya Robert Mugabe. Huko vilishuhudiwa vitendo vya matumizi ya nguvu kutoka mwaka 2000 pale mashamba ya wazungu yalipotwaliwa kwa nguvu, hali iliyopelekea uchumi wa nchi kuanguka chini na mazao ya kilimo kuwa haba.

Itakumbukwa kwamba katika miaka ya mwisho ya utawala wake, Mugabe alikiri kwamba zoezi la marekebisho ya ugawaji wa ardhi katika nchi yake lililopelekea mashamba makubwa ya wazungu katika nchi hiyo kupewa wakulima wa Kiafrika lilikwenda kombo.

Alitoa sababu kwamba mashamba hayo yalikuwa makubwa mno kwa watu hao, hivyo kutoweza kuyaangalia vizuri. Pia alisema siasa za ardhi zilikuwa hazijafikiriwa vizuri kabla ya mashamba hayo kugawiwa kwa Waafrika.

Hata hivyo, Mugabe mwenyewe pia alilaumiwa kwamba mashamba yaliochukuliwa kutoka kwa Wazungu walipewa marafiki zake wa kisiasa, na wengi wao waliofaidika hawakupewa vifaa vya kulimia na pia mafunzo ili kuweza kulima kwa faida.

Licha ya hayo yote, tatizo la kushindwa marekebisho ya umiliki nchini Zimbabwe lilitokana na Serikali ya Uingereza (mkoloni wa zamani wa Zimbabwe), chini ya waziri mkuu Tony Blair, kuachana na ule utaratibu uliokubaliwa na mtangulizi wake, Margret Thatcher, kwa kuitupilia ile ahadi ya kutoa nusu ya fedha za kuyanunua mashamba ya wazungu katika Zimbabwe huru kwa msingi wa kuuza na kununua kwa hiyari. Serikali ya Mugabe ilijibu kwa kuyataifisha mashamba ya wazungu bila ya kulipa fidia, hivyo kuweko uhasama baina ya Uingereza na Zimbabwe hadi pale alipoondolewa Mugabe hivi karibuni.

Afrika Kusini inatajika duniani kuwa ni nchi ilio na tafauti kubwa ya mgao wa vipato kati ya wakazi wake. Katika nchi hiyo yenye makabila mengi na ambayo iliingia katika mfumo wa demokrasia mwaka 1994, kwa mujibu wa tarakimu rasmi, ni kwamba asilimia 55 ya wakazi wanaishi ndani ya dimbwi la umaskini.

Rais Ramaphosa ana matatizo pomoni mbele yake hadi uchaguzi mkuu wa mwakani na hata baada ya uchaguzi huo, pindi chama chake cha ANC kitashinda.

Kutwaa mashamba binafsi na kuyagawa kwa Waafrika walio maskini haitakuwa dawa ya kila kitu. Rais huyo ameichukua nchi ikiwa katika hali ngumu; uchumi umekwama, ukosefu wa ajira ni mkubwa.

Rais Zuma aliyeondoka madarakani ameiacha hali ya nchi imefilisika kifedha na kimorali pia. Yeye pamoja na marafiki zake katika ANC walijitajirisha huku Waafrika wengi wakiendelea kuishi katika umaskini.

Pia Ramaphosa inambidi akipe uhai mpya chama chake cha ANC na nchi nzima pia. Kwa wana ANC, chama chao na nchi ni kitu kimoja, hawatenganishi. Kwa Waafrika Kusini wengi suala ni ama ANC ina haki bado ya kutawala au Afrika Kusini inabidi ikombolewe kutokana na vuguvugu la ukombozi.

Huenda sasa Ramaphosa, kati ya viongozi wa ANC, anafaa kuongoza na kuanzisha mchapo mpya wa kuwapa Waafrika pia uwezo wa kiuchumi na si tu wa kisiasa peke yake.

Yeye ni mjanja, mchangamfu pia, na hajafungamanishwa na rushwa hadi sasa. Watu kama yeye si wengi ndani ya ANC. Pia yeye ana marafiki wengi zaidi nje ya ANC yenyewe.

Alishinda kura kwa wingi wa chupuchupu kuwa mkuu wa chama hapo Desemba mwaka jana. Huenda kwa vile watu wengi ndani ya chama hawamjui vilivyo alivyo, na hawajui wapi atakielekeza chama na ataielekeza nchi. Hiyo huenda ni faida kwa upande wake.

Chanzo: Mwananchi
 
Mtamudu kuendesha kilimo au mpewe ardhi na kuanza kujenga vijumba vya udongo na ajira mnajikosesha.
 
South Afrika wawe makini sana na hii isue ya Ardhi.
Sema CR anajua uchumi kwa hiyo sidhani kama italeta shida
 
Wakifanya pupa SA inakuja kuwa maskini kupindukia maana hao KhoiSan na Wabantu waliobaki hawana tofauti na watu wa Pwani ya Tanzania. Nadhani sifa zetu sisi wa Pwani mnatujua.
 
Sisi mamwinyi
Nalog off
 
View attachment 706550

"Let us all agreed that Black people cannot rule themselves, Whites are born in order to rule, and Blacks are born to be ruled."

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.

Kwa kiasi fulani hivi hao Watu weusi wa nchi hiyo ya Afrika Kusini wanaweza kuwa wapo sahihi, Ila hofu yangu kubwa ipo juu ya namna ya Utekelezaji wa Mkakati huo wa Utwaaji wa Ardhi. Je, Mpango wa kutekeleza jambo hili upo vizuri?
Najua lazima Mpango huo utakuwa mbaya sana na utaleta matokeo hasi mabaya sana kwa nchi hiyo ya Afrika Kusini.

Mathalani, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wakati huo alipokuwa anawapokonya Ardhi raia Wazungu kwenye nchi hiyo alikuja na Sera yake iliyokuwa ikisema kwamba Mtu mmoja anapaswa amiliki shamba moja tu na wala siyo zaidi, yaani: "One Man One Farm." Lakini matokeo yake yeye mwenyewe Mugabe alijitwalia na kujigawia Mashamba mengi yapatayo 28 nchi nzima hali iliyosababisha manung'uniko katika jamii na yeye Rais kuingia kwenye migogoro mikubwa na washirika wake wa karibu Sana kwenye Utawala wake kama vile Mwanasheria Mkuu wa Serikali yake na Mkuu wake wa Majeshi
 
View attachment 706550

Wabunge 241 wa Afrika Kusini wameukubali na wengine 81 kuupinga muswada wa kutaka kutwaliwa na kununuliwa ardhi kwa nguvu katika nchi hiyo.

Hadi Agosti 30 mwaka huu, Kamati ya Bunge la nchi hiyo imetakiwa ichunguze kama mabadiliko ya Katiba yanawezekana ili Serikali iweze kutwaa ardhi za watu binafsi.

Muswada huo hapo kabla uliwasilishwa na chama cha mrengo mkali wa shoto, Wapiganaji wa Ukombozi wa Kiuchumi (EFF).

“Wakati wa maridhiano umepita. Sasa umefika wakati wa kutolewa haki,” alisema kiongozi wa EFF, Julius Malema.

Aliwaelezea wakoloni wa zamani wa Kiholanzi huko Afrika Kusini kuwa ni “wahalifu waliotunyang’anya ardhi yetu”.

Alisema wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi, vizazi vyao viliwatenga na kuwabakisha Waafrika katika makambi ya vizuizi ambayo leo yanaitwa mitaa ya Waafrika.

Muswada huo pia umeungwa mkono kwa wingi na wabunge wa Chama Tawala cha ANC. Katika mkutano wake mkuu Desemba mwaka jana, chama hicho kilitangaza msimamo mkali kuhusu suala la kugawa ardhi. Kwa vile kuna uchaguzi mkuu mwakani, chama hicho kinajikuta hivi sasa katika mbinyo. Na ilivyokuwa sasa kimeukubali muswada huo inawezekana kikaungwa mkono na wapiga kura wengi zaidi miongoni mwa raia wa Kiafrika walio maskini.

Mbunge Thandeka Mbabama aliuelezea uamuzi huo kuwa ni mbinu ya kubadilisha dira, kujaribu kuyafumbia macho makosa yaliyofanywa hapo kabla na ANC.

Rushwa na ufisadi pamoja na kushindwa kuwapatia wakulima wa Kiafrika mafunzo na vifaa ndio kizingiti kikubwa cha kuleta marekebisho ya ardhi yaliyoahidiwa na chama hicho katika ilani zake za uchaguzi za hapo kabla.

Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Afrika Kusini umegundua kwamba robo tatu ya ardhi ya kilimo iko mikononi mwa wakulima wa Kizungu, si kidogo kama walivyokuwa nayo mwishoni mwa utawala wa kibaguzi. Wakati huo walishikilia asilimia 85. Lakini bado haijulikani lini Bunge litajadiliana juu ya mabadiliko haya ya katiba.

Shauri hilo la kutwaa mashamba, na ikilazimika bila kulipa fidia inayostahiki, limepingwa na wakulima.

Rais wa Shirikisho la jumuiya za wakulima wa Afrika Kusini, Agri SA, Dan Kriek amesema hatua hiyo haiingii akilini, kwani inaumiza uchumi wa mabenki ambayo yamewekeza sana katika kilimo. Alisema hoja kama hizo za kimsingi hazijatiliwa sana maanani katika mdahalo, na pia ni kwamba wazungu na Waafrika wote wana haki ya kumiliki mali katika nchi hiyo.

Suala la kutaka kutwaliwa ardhi limekuwa tete katika Afrika Kusini tangu kumalizika kipindi cha ubaguzi. Katika hotuba yake ya kwanza tangu alipokamata urais wa nchi hapo Februari mwaka huu, Cyril Ramaphosa aliunga mkono kutwaliwa mashamba hata bila ya kulipwa fidia, ila tu uzalishaji wa mazao ya kilimo, hasa yale ya vyakula, upande. Aliahidi kwamba ataharakisha Waafrika wanagawiwa ardhi.

Sababu kubwa ya kuchukuliwa hatua hii hivi sasa ni kwamba, licha ya kupita miaka 24 tangu kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi katika Afrika Kusini, bado sehemu kubwa ya ardhi ya kilimo katika nchi hiyo imo mikononi mwa wakulima wa Kizungu.

Kuna utafiti mwingine ulioonyesha kwamba licha ya wazungu wa Afrika Kusini kuwa ni asilimia tisa tu ya wakazi, lakini wao wanamiliki asilimia 73 ya ardhi inayotumiwa kwa kilimo.

Hata hivyo, wahakiki wanahofia kwamba uamuzi huu wa Afrika Kusini katika siasa yake ya maendeleo unaweza ukaielekeza nchi hiyo katika ile njia iliyofuatwa na nchi jirani ya Zimbabwe chini ya Robert Mugabe. Huko vilishuhudiwa vitendo vya matumizi ya nguvu kutoka mwaka 2000 pale mashamba ya wazungu yalipotwaliwa kwa nguvu, hali iliyopelekea uchumi wa nchi kuanguka chini na mazao ya kilimo kuwa haba.

Itakumbukwa kwamba katika miaka ya mwisho ya utawala wake, Mugabe alikiri kwamba zoezi la marekebisho ya ugawaji wa ardhi katika nchi yake lililopelekea mashamba makubwa ya wazungu katika nchi hiyo kupewa wakulima wa Kiafrika lilikwenda kombo.

Alitoa sababu kwamba mashamba hayo yalikuwa makubwa mno kwa watu hao, hivyo kutoweza kuyaangalia vizuri. Pia alisema siasa za ardhi zilikuwa hazijafikiriwa vizuri kabla ya mashamba hayo kugawiwa kwa Waafrika.

Hata hivyo, Mugabe mwenyewe pia alilaumiwa kwamba mashamba yaliochukuliwa kutoka kwa Wazungu walipewa marafiki zake wa kisiasa, na wengi wao waliofaidika hawakupewa vifaa vya kulimia na pia mafunzo ili kuweza kulima kwa faida.

Licha ya hayo yote, tatizo la kushindwa marekebisho ya umiliki nchini Zimbabwe lilitokana na Serikali ya Uingereza (mkoloni wa zamani wa Zimbabwe), chini ya waziri mkuu Tony Blair, kuachana na ule utaratibu uliokubaliwa na mtangulizi wake, Margret Thatcher, kwa kuitupilia ile ahadi ya kutoa nusu ya fedha za kuyanunua mashamba ya wazungu katika Zimbabwe huru kwa msingi wa kuuza na kununua kwa hiyari. Serikali ya Mugabe ilijibu kwa kuyataifisha mashamba ya wazungu bila ya kulipa fidia, hivyo kuweko uhasama baina ya Uingereza na Zimbabwe hadi pale alipoondolewa Mugabe hivi karibuni.

Afrika Kusini inatajika duniani kuwa ni nchi ilio na tafauti kubwa ya mgao wa vipato kati ya wakazi wake. Katika nchi hiyo yenye makabila mengi na ambayo iliingia katika mfumo wa demokrasia mwaka 1994, kwa mujibu wa tarakimu rasmi, ni kwamba asilimia 55 ya wakazi wanaishi ndani ya dimbwi la umaskini.

Rais Ramaphosa ana matatizo pomoni mbele yake hadi uchaguzi mkuu wa mwakani na hata baada ya uchaguzi huo, pindi chama chake cha ANC kitashinda.

Kutwaa mashamba binafsi na kuyagawa kwa Waafrika walio maskini haitakuwa dawa ya kila kitu. Rais huyo ameichukua nchi ikiwa katika hali ngumu; uchumi umekwama, ukosefu wa ajira ni mkubwa.

Rais Zuma aliyeondoka madarakani ameiacha hali ya nchi imefilisika kifedha na kimorali pia. Yeye pamoja na marafiki zake katika ANC walijitajirisha huku Waafrika wengi wakiendelea kuishi katika umaskini.

Pia Ramaphosa inambidi akipe uhai mpya chama chake cha ANC na nchi nzima pia. Kwa wana ANC, chama chao na nchi ni kitu kimoja, hawatenganishi. Kwa Waafrika Kusini wengi suala ni ama ANC ina haki bado ya kutawala au Afrika Kusini inabidi ikombolewe kutokana na vuguvugu la ukombozi.

Huenda sasa Ramaphosa, kati ya viongozi wa ANC, anafaa kuongoza na kuanzisha mchapo mpya wa kuwapa Waafrika pia uwezo wa kiuchumi na si tu wa kisiasa peke yake.

Yeye ni mjanja, mchangamfu pia, na hajafungamanishwa na rushwa hadi sasa. Watu kama yeye si wengi ndani ya ANC. Pia yeye ana marafiki wengi zaidi nje ya ANC yenyewe.

Alishinda kura kwa wingi wa chupuchupu kuwa mkuu wa chama hapo Desemba mwaka jana. Huenda kwa vile watu wengi ndani ya chama hawamjui vilivyo alivyo, na hawajui wapi atakielekeza chama na ataielekeza nchi. Hiyo huenda ni faida kwa upande wake.

Chanzo: Mwananchi
Trump yupo sahihi
 
Back
Top Bottom