Mashamba yanapatikana Kiwangwa


Malila,
Vipi kwa upande wa kuelekea Mkuranga? Uzoefu wako ukoje huko? Yaani upatikanaji wa mashamba na ubora wa ardhi yenyewe?
 
Malila,
Vipi kwa upande wa kuelekea Mkuranga? Uzoefu wako ukoje huko? Yaani upatikanaji wa mashamba na ubora wa ardhi yenyewe?

Natembea nuruni kabisa,
Mkuranga ktk vijiji vya Msorwa ( 60Km from Tazara), Shungubweni (67km from Tazara),Mpafu, kuna ardhi nzuri bado kwa ufugaji kwa sababu kuna maji ya kutosha ya mito au kuchimba visima vifupi. Bei zinacheza kati ya 250 mpaka 450 kwa eka. Na sehemu zenye kichanga unaweza pata kwa 200 kamili kwa eka.

Kando ya mito kuna kilimo cha matikiti,mpunga na mboga kama nyanya, pilipili, matango nk. Kididimo kuna ardhi nzuri sana kunafaa kwa mihogo na mazao mengine. Mbezi/Msufini kuna ardhi yenye rutuba sana,ila vijiji hivi havina maji ila viko ktk barabara kuu ya kisiju.

KimanziChana/Mkiu/Mkamba kuna ardhi bomba sana kwa kilimo cha Mpunga,Mahindi,Choroko, na mvua huko zinanyesha vizuri, kama kawaida zikigoma ni hatari tupu. Vijiji hivi vinakabiliwa na tatizo la maji. Huu upande wa Hoyoyo kuna ardhi kubwa na nzuri ila ukame ukipita unaweza kupata ugonjwa ghafla.

Ila kuanzia Vikindu mpaka Mwalusembe kando ya barabara kuu, bei zimepanda ajabu, sababu ya viwanda vinavyojengwa kwa wingi kando ya barabara hii ya kusini. Eka inafika milioni 30 na kuendelea. Pale Mwanambaya niliuliza eka saba ni sh ngapi,nikaambiwa nitoe milioni 80 hivi, hiyo ni january 2012. Juzi Mchina kachukua kwa 100M.
 
Asante Malila kwa taarifa inayojitosheleza vizuri.
 

Hatuumizani Mkuu, Ni kukubali kuburuzwa... Mi bei za Ajabu ajabu sinunui hata iweje, labda uniambie ni mgodi... Kuna watu wengi sana wako desperate na ununuzi wa ardhi na hao ndio wanaosababisha bei zipande... otherwise.. Kununua heka moja kwa Milioni Moja tu na huku huna mkakati maridhawa wa kuliendeleza kwa kilimo, ufugaji, au makazi basi ni sawa na kuweka hela shimoni siku ukiwa na shida ukazitoe wakati hapo shimoni panaweza kutokea lolote lile... Hivi kuna kesi ngapi za watu kununua maeneo ya gharama kubwa na kuwekeza halaf serekali yetu yenye sera za kukurupuka inakuja kupima viwanja na kuwagawia waliowakuta/wenye mali viwanja viwili vitatu na kuwacharge tozo pungufu kwa sq meter?? huku wakishuhudia mahekari yao yakiuziwa wengine kwa malengo tofauti na waliyojiwekea..
Mi naona Kumiliki Ardhi Si Tatizo, Lakini Tatizo ni kulimbikiza Ardhi usizozitumia...
Binafsi namuona mwenye ardhi yenye ukubwa wa heka mbili tu lakini anazalisha tani kumi kwa mwaka za mazao yeyote ni Mtu bora na mwema kwa jamii kuliko yule mwenye pori (virgin) lenye hekari elfu moja lisilotumika kwa matumizi yeyote yale....
Ni papara zetu tu ndio zinazotusababishia haya...
Eti heka moja milioni tano, Hivi hela zinaokotwa eeh??? Mbona TZ ina maeneo ya kutosha tu, hata tukisema tugawane heka mbili mbili taifa zima haziishi.
 

Hahah Mkuu hapa umenikumbusha hotuba za MAgufuli....
 
Kwa Kiwangwa na upatikanaji wa mashamba kwa Bei hiyo ya 250,000 ni sahihi huyu bwana asemacho; mimi mwenyewe shahidi nishawahi enda huko tena si chini ya mara mbili kwa ajili ya kutafuta mashamba, ila sema yapo kwa ndani kidogo na barabara yapata km 8 na kuendelea ingawa hata ya barabarani yanapatikana ila bei yake iko juu na sio mashamba makubwa.
Uwepo wa lami kule ndio unawazindua wakazi wa kule wanaanza kujanjaruka hasa pale watu wengi watokao mjini tunavyo kimbilia mashamba na kuyanunua kwa wingi wanapandisha bei kidogo wanaweza kukuanzia laki 5 lkn ni wepesi kushuka wala hutumii nguvu nyingi kubargain; Kuna jamaa anaitwa Same ni mwenyeji wa huko namba yake ya simu ni 0684949860.
Mie nshafanya naye biashara na kaniuzia shamba la Ekari nne mbele kidogo ya Kiwangwa stand kama km 10 hivi, hivyo apendaye anaweza mcheki akampa msaada, ila anajua sana kuupepeta huyo jamaa ni mzaramo haswaa!!!
 
Shamba la ndanindani sio lenyewe kwa kufichia magendo na zile nyara zangu nilizoiba siku nyingi... Naomba uni pm hiyo no ya mzeee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…