Mashambulio ya kujitoa muhanga je ilikuwa kweli au propaganda?

Mashambulio ya kujitoa muhanga je ilikuwa kweli au propaganda?

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Nakumbuka enzi hizo nikiwa mdogo miaka ya 2000+ nilikuwa napenda sana kusikiliza BBC yaani nilikuwa sipitwi. Moja kati ya habari nazozikumbuka ni watu kuvaa mabomu kujitoa muhanga sijui sokoni, kwenye kituo cha basi n.k .

Nakumbuka hizo habari zilikuwa zinatoka sana sana Afghanistan, Iraq na Pakistán.

Baada ya kuja kwa mitandao ya kijamii, sasahivi hatutegemei BBC tena kwa habari .Lakini kutokana na jinsi haya matukio ya kujitoa muhanga yalivyokuwa yanatangazwa na BBC karibia kila siku nilitegemea media nyingine zilizopo ziendelee kutangaza kama kweli yapo.

Cha kushangaza,siyasikii tena hadi najiuliza au walipokuwa wanagawa mabomu ya kujitoa muhanga hawagawi tena?

Lakini nikawaza pia au ni propaganda nyingine za BBC zilizokuwa zinajazwa vichwani mwetu kabla ya ujio wa mitandao ya kijamii?

NB: Si kwa lengo la kukashifu Imani ya mtu mwingine maana kuna watu wataanza kushambulia dini za watu.
 
Sema tu umekuwa shallow sana kufuatilia mambo

Hukumbuki miaka michache iliyopita wanariadha wa Olympic kule Uingereza walishambuliwa na mabomu kwa kujitoa muhanga?

Japo waarabu wamebadilika kidogo ila bado matukio yapo
 
Unajua maisha ya binadamu tunapitia hatua na vipindi tofauti tofauti.

Zamani watu waliabudu mizimu na kutoa kafara za binadamu wenzao kwa kuchinjwa au kuchomwa moto ukiwa hai, maana yake kwamba wanatoa sadaka kwa Miungu.

Baadae sana hivyo vipindi na zama zake zikapita.
Kwahiyo hata hilo la kujilipua eti kisa kuna mabikira sehemu wanakusubiria lilikuwepo na huenda zama zake ndiyo zinaishia,
The same kama watu wanavyozidi kuacha kujihusisha na dini.
Binadamu miaka ya baadae wataishi kwa kutegemea fact na siyo imani tena.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada. Nakumbuka enzi hizo nikiwa mdogo miaka ya 2000+ nilikuwa napenda sana kusikiliza BBC yaani nilikuwa sipitwi. Moja kati ya habari nazozikumbuka ni watu kuvaa mabomu kujitoa muhanga sijui sokoni, kwenye kituo cha basi n.k . Nakumbuka hizo habari zilikuwa zinatoka sanasana Afghanistan, Iraq na Pakistán.
Baada ya kuja kwa mitandao ya kijamii, sasahivi hatutegemei BBC tena kwa habari .Lakini kutokana na jinsi haya matukio ya kujitoa muhanga yalivyokuwa yanatangazwa na BBC karibia kila siku nilitegemea media nyingine zilizopo ziendelee kutangaza kama kweli yapo. Cha kushangaza,siyasikii tena hadi najiuliza au walipokuwa wanagawa mabomu ya kujitoa muhanga hawagawi tena?
Lakini nikawaza pia au ni propaganda nyingine za BBC zilizokuwa zinajazwa vichwani mwetu kabla ya ujio wa mitandao ya kijamii?
NB: Si kwa lengo la kukashifu Imani ya mtu mwingine maana kuna watu wataanza kushambulia dini za watu.
Propaganda dhidi ya nani ?.....huko Afghanistan baada ya Taliban kurudi madarakani hayo mashambulizi yamepungua ila Pakistan bado yanatokea mara nyingi tu.
 
Ata yanayoendelea Congo...wajuba wakishashiba hutasikia tena hizo kelele
 
Sema tu umekuwa shallow sana kufuatilia mambo

Hukumbuki miaka michache iliyopita wanariadha wa Olympic kule Uingereza walishambuliwa na mabomu kwa kujitoa muhanga?

Japo waarabu wamebadilika kidogo ila bado matukio yapo
Asante kwa ufafanuzi
 
Fuatiria taarifa vzr acha kushinda betting,kobaxi hawajaacha kujitoa muhanga kisa pombe,kitimoto na kulombana akhera.
 
Back
Top Bottom