Masharti ya kuuza Petroli dukani kijijini.

Rapture Man

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Posts
439
Reaction score
145
Hello Wadau, niko kijijini, hapa kupata petroli ni shida. Natafakari kufungua duka la kuuza petroli kwa rejareja, sio kufungua petrol station. Naomba mnifahamishe sheria na taratibu zinasemaje. Mfano, bei itapangwa na ewura au nitajipangia mwenyewe? Leseni nitapata kivipi au nakata leseni ya kawaida kama biashara zingine? Je kuna standard zozote za ku-store hiyo petrol na kupima volume during retail sale au naweza tumia chupa za uhai za lita 1 kuwapimia wateja? TRA sio issue, kodi ya mapato ni lazima kulipa. Asanteni. Wenu Mchakalikaji.
 
Ingawa sina uhakika huwa naona vi pump na storage tank chini. Pia kuna umbali kidogo na nyumba au majengo mengine. Imagine uiweke kwenye viduka na mtu aje na sigara!
 
hiyo biashara ndogo sana achana na kuipambiza longolongo hizo! kilichopo we tafuta dumu zako 10 za 20ltrs nenda petrol station yeyote nunua shehena yako kisha mkabidhi dogo apime kwenye vibobo(1lt& 0.5lt) utauza kwa 2500/ltr na 1300 kwa nusu ltr. Hakuna atakaekuzingua ila ukitaka complications itakula kwako coz wajinga ndio waliwao.
 
Asante Mama Joe na Kisima kwa michango yenu yenye kujenga.
 
Wala hio biz haina complications wala nini.. Just do it
 
km una duka weka nje tu,
barabarani yanakopita magari na pikipiki
maana yangu usije ukaingiza ndani ya nyumba ni hatari moto wake
 
Hello Wadau, niko kijijini, hapa kupata petroli ni shida. Natafakari kufungua duka la kuuza petroli kwa rejareja, sio kufungua petrol station. Naomba mnifahamishe sheria na taratibu zinasemaje. Mfano, bei itapangwa na ewura au nitajipangia mwenyewe? Leseni nitapata kivipi au nakata leseni ya kawaida kama biashara zingine? Je kuna standard zozote za ku-store hiyo petrol na kupima volume during retail sale au naweza tumia chupa za uhai za lita 1 kuwapimia wateja? TRA sio issue, kodi ya mapato ni lazima kulipa. Asanteni. Wenu Mchakalikaji.

Pamoja na ukweli kwamba ndio unaanza, tahadhari za usalama ni lazima sana kwako mwenyewe na mazingira yako. Kama mtaji wako uko vizuri, andaa sehemu salama na iwe well secured,kisha nunua vile vitank vya chuma vya lita mpaka 500 hivi, kama ukishindwa tumia madumu au mapipa ya chuma. Kisha pata ushauri toka jamaa wa fire brigade walio karibu.

Hata kama ni kijijini na mtaji ni mdogo, usifanye kienyeji sana kama kuanika mbele ya nyumba au kuweka barabarani kwenye jua. Pia waweza kuwatembelea dealers wengine ukaomba ushauri na ujuzi pia. Napata hofu sana na tabia ya kuuza petrol barabarani kama vile njugu au karanga.

Ukipita njia ya Msata, kuanzia Bagamoyo mpaka Kiwangwa, njiani ni petrol tupu imeanikwa!!!!
 
Ni hicho tu hata mie nahofia, kuna familia waliungua mtu na mkewe na kufa usiku wakitunza petrol sebuleni wakiacha watoto 9 first std 5 hadi leo sisahau. Jenga au weka mbali kidogo na frame au nyumba.
Pamoja na ukweli kwamba ndio unaanza, tahadhari za usalama ni lazima sana kwako mwenyewe na mazingira yako. Kama mtaji wako uko vizuri, andaa sehemu salama na iwe well secured,kisha nunua vile vitank vya chuma vya lita mpaka 500 hivi, kama ukishindwa tumia madumu au mapipa ya chuma. Kisha pata ushauri toka jamaa wa fire brigade walio karibu.

Hata kama ni kijijini na mtaji ni mdogo, usifanye kienyeji sana kama kuanika mbele ya nyumba au kuweka barabarani kwenye jua. Pia waweza kuwatembelea dealers wengine ukaomba ushauri na ujuzi pia. Napata hofu sana na tabia ya kuuza petrol barabarani kama vile njugu au karanga.

Ukipita njia ya Msata, kuanzia Bagamoyo mpaka Kiwangwa, njiani ni petrol tupu imeanikwa!!!!
 
Mavado, Ukwaju, Malila, and again, Mama Joe, thank you very much. I see light at the end of the tunnel. Hizo tank za chuma za lita 500 ndio zile zinazotengenezwa kienyeji nadhani? Hua naona zinatumiwa na wauza mafuta ya taa.
Vipi kama nikichimbia pipa la chuma ardhini? Najua nitahitaji pump ndogo ingawa usalama ndio kitu cha kwanza.
 
Hello Wadau, niko kijijini, hapa kupata petroli ni shida. Natafakari kufungua duka la kuuza petroli kwa rejareja, sio kufungua petrol station. Naomba mnifahamishe sheria na taratibu zinasemaje. Mfano, bei itapangwa na ewura au nitajipangia mwenyewe? Leseni nitapata kivipi au nakata leseni ya kawaida kama biashara zingine? Je kuna standard zozote za ku-store hiyo petrol na kupima volume during retail sale au naweza tumia chupa za uhai za lita 1 kuwapimia wateja? TRA sio issue, kodi ya mapato ni lazima kulipa. Asanteni. Wenu Mchakalikaji.

Mkuu uko maeneo gani..??? Njoo Inbox tufanye Biashara. Tuna Magari yenye tank na Pump nyuma. Tutakupa Gari ila mafuta unanunua kwetu
 
Weka peupe, hujui kwamba hili deal kwa sasa linatafutwa na wengi sana, juzi nilikuwa naongea na dealer wa PUMA Makambako kujua ni nini cha kufanya kwa dealers wadogo wadogo wa vijijini. Nafahamu kuna vile vitenka vidogo vya mafuta, vipo vinasambaza mafuta ya taa majumbani.

Ainisha ujazo wa gari na gharama zake ili hata huyu mwenye uzi akishindwa wengine wapo watakufuata.
 
Mkuu uko maeneo gani..??? Njoo Inbox tufanye Biashara. Tuna Magari yenye tank na Pump nyuma. Tutakupa Gari ila mafuta unanunua kwetu

komunteeee....uko nchi gani? jibu hoja na maswali ya wadau.
 
Back
Top Bottom