Rapture Man
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 439
- 145
Hello Wadau, niko kijijini, hapa kupata petroli ni shida. Natafakari kufungua duka la kuuza petroli kwa rejareja, sio kufungua petrol station. Naomba mnifahamishe sheria na taratibu zinasemaje. Mfano, bei itapangwa na ewura au nitajipangia mwenyewe? Leseni nitapata kivipi au nakata leseni ya kawaida kama biashara zingine? Je kuna standard zozote za ku-store hiyo petrol na kupima volume during retail sale au naweza tumia chupa za uhai za lita 1 kuwapimia wateja? TRA sio issue, kodi ya mapato ni lazima kulipa. Asanteni. Wenu Mchakalikaji.
Pamoja na ukweli kwamba ndio unaanza, tahadhari za usalama ni lazima sana kwako mwenyewe na mazingira yako. Kama mtaji wako uko vizuri, andaa sehemu salama na iwe well secured,kisha nunua vile vitank vya chuma vya lita mpaka 500 hivi, kama ukishindwa tumia madumu au mapipa ya chuma. Kisha pata ushauri toka jamaa wa fire brigade walio karibu.
Hata kama ni kijijini na mtaji ni mdogo, usifanye kienyeji sana kama kuanika mbele ya nyumba au kuweka barabarani kwenye jua. Pia waweza kuwatembelea dealers wengine ukaomba ushauri na ujuzi pia. Napata hofu sana na tabia ya kuuza petrol barabarani kama vile njugu au karanga.
Ukipita njia ya Msata, kuanzia Bagamoyo mpaka Kiwangwa, njiani ni petrol tupu imeanikwa!!!!
Hello Wadau, niko kijijini, hapa kupata petroli ni shida. Natafakari kufungua duka la kuuza petroli kwa rejareja, sio kufungua petrol station. Naomba mnifahamishe sheria na taratibu zinasemaje. Mfano, bei itapangwa na ewura au nitajipangia mwenyewe? Leseni nitapata kivipi au nakata leseni ya kawaida kama biashara zingine? Je kuna standard zozote za ku-store hiyo petrol na kupima volume during retail sale au naweza tumia chupa za uhai za lita 1 kuwapimia wateja? TRA sio issue, kodi ya mapato ni lazima kulipa. Asanteni. Wenu Mchakalikaji.
Mkuu uko maeneo gani..??? Njoo Inbox tufanye Biashara. Tuna Magari yenye tank na Pump nyuma. Tutakupa Gari ila mafuta unanunua kwetu