Pre GE2025 Masheikh 12 waliochiwa na mahakama kutokana na tuhuma za ugaidi Machi 4 wakamatwa tena na kurudishwa gerezani!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu, mambo yameamka huku

====

Jana Machi 4, 2025 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji Kirekiano iliwaachia huru MASHEIKH 12, walio kaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi.

Baada ya hukumu hiyo Shura ya Maimamu Tanzania ilitoa taarifa ya kuachiwa huru Masheikh hao.

Wakati taarifa hiyo ikitolewa Masheikh hao walikua wako chini ya itifaki za watu wa usalama na ndugu walitakiwa kwenda kituo cha Polisi cha stakishari kwaajili ya kukamilisha itifaki hizo.

Hata hivyo majira ya magharibi ndugu walipofika stakishari waliambiwa masheikh hao hawajafikishwa pale.

Aidha leo asubuhi ndipo zilipopatikana taarifa kuwa ndugu Masheikh hao wapo katika gereza la Ukonga walilpokuwapo awali.

Ni wazi baada ya Mahakama kuwaachia huru Masheikh hao, watu wa usalama walitumia mbinu mbalimbali wakafanikiwa kuwakamata tena na kuwafungulia mashtaka mapya bila ya ndugu zao kufahamu.

Kwa hakika tukio hili linadhihirisha jinsi ambavyo serikali iliyopo madarakani isivyojali haki za binadamu. Watu hawa wamekamatwa toka 2015, mpaka leo serikali imeshindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yao lakini inaendelea kuwanyima haki za msingi na kuwatesa.

Pia soma: Pre GE2025 - Masheikh 12, waliokaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi waachiwa huru

Katika taarifa ya jana tumeeleza madhila yaliyowakuta baadhi yao ikiwa ni pamoja na kupoteza wenziwao na wengine kufia gerezani.


Hivi viongozi wetu wanashindwa kuvihoji vyombo vyao juu ya matukio haya yaliyo kinyume na sheria na utu.

Hivi inaingia akilini mzee Sleiman Ulatule miaka 90, achukue familia yake ya zaidi ya watu 7, waende kuvamia kituo cha polisi?


Katika wasifu huo watawala watakua na uso gani wa kusimama mbele ya wananchi wakiwemo Waislamu kuwaomba ridhaa ya kuongoza nchi.

Ni zuzu wa kiasi gani atakayewapa ridhaa watawala wasio zingatia haki za binadamu, uhuru na haki za kuishi zinazolindwa na Katiba ya nchi.


Aidha tutumie fursa hii kuwaomba Waislamu wote nchini kutumia fursa hii ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuomba dua makhsusi na kumkabidhi Mwenyezi Mungu Mtukufu atoe hukumu kwa haya wanayotendewa wanyonge nchini Tanzania.

Atakayeacha kuomba dua hii maana yake ameridhia haya wanayotendewa binadamu wenzake wasio na hatia yoyote.


Shura ya Maimamu Tanzania
 
watu wana tuhuma za ugaidi, na shura ya maimamu inawatetea. tuweke conclusion gani hapo?
 
Hao wataachowa karibu na uchaguzi na itatangazwa kuwa ni huruma ya bibi Chura Kiziwi.
 
Watu hawajaelewa. Ndio mashekhe wale wameachiwa, ila kuna vitu vinahitajika kukamilisha kuachiwa kwao. Hata mahakamani hawakufika walikua bado gerezani. Watafikishwa au kuachiwa moja kwa moja kutoka gerezani, msidanganyike.
 
watu wana tuhuma za ugaidi, na shura ya maimamu inawatetea. tuweke conclusion gani hapo?
What are you insinuating? Kwamba Shura ya Maimam nao ni magaidi au walikuwa part and parcel ya huo ugaidi uliowasababisha hao maimam kuwa gerezani?
Whatever it is, miaka yote hiyo how come jamaa hao bado ni remandees? Ni upelelezi gani wa miaka 10?
 
Tanzania ndiyo Nchi pekee Duniani ambayo unaweza kukamatwa Kwa kosa lisilojulikana kisha ukasota jela miaka hata 10 ukiambiwa Uchunguzi haujamilika.

Sasa unakaaje na mtu jela miaka 10 plus bila uchunguzi kukamilika wa tuhuma zake.

Kulikuwa na haja gani ya kumkamata mtu kama hauna vithibitisho vya mashtaka yake??
 
Ukiona hivi ujue jamaa ni very dangerous, hawana sababu ya kuwafanyia hivi kama sio imminent threat to national security .
Then bora watafute namna to convict them, this shit of them staying in the pen for ten years is tormenting them mentally and depressing with a lot of uncertainties. It's a bloody fatal mental torture.
Ten years as a remandee equals the sentence of 15yrs, whilst a remandee is presumed innocent until proven guilty now imagine all those damn years staying without being sure what will be your fate.
 
watu wana tuhuma za ugaidi, na shura ya maimamu inawatetea. tuweke conclusion gani hapo?
Mzee ulivokutana na zile tuhuma za kubakwa,unataka yule aliyetuhumiwa kukuingilia kinguvu asitetewe?........Si ndio maaa Kuna mahakama kuthibitisha uhalali wa makosa?
 
Nasimama na Serikali
Serikali na usalama wa Taifa hawawezi kuwaonea tu
Kuna kitu kikubwa na mipango miovu wanayo
 
Ukiona hivi ujue jamaa ni very dangerous, hawana sababu ya kuwafanyia hivi kama sio imminent threat to national security .
Acheni chuki zenu. Huu ni uhuni wa serikali. Kama ni hatari kwa nini wasingekutwa na hatia na wanakaa tu gerezani? Angalia sana hujui kesho ni nini kinakuja kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…