Masheikh wa Afrika ya Mashariki walipokusanyika kumuombea dua Abbas Sykes

Masheikh wa Afrika ya Mashariki walipokusanyika kumuombea dua Abbas Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MASHEIKH WA AFRIKA YA MASHARIKI WALIPOKUSANYIKA KUMUOMBEA DUA ABBAS SYKES

Nipo nyumbani baada ya Maghrib akaja Sheikh Mahdi kaniletea picha adhim kupita kiasi.

Sheikh Mahdi ni mtoto wa Sheikh Muharam Saleh ambae ni miongoni mwa wanafunzi wa Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika.

Sheikh Mahdi akakaa kitako na mimi kama unavyoons kwenye picha kunipa majina ya masheikh hawa wote nami nayaweka hapo chini:

1. …
2. Sheikh Haji Sadiki
3. Maalim Said bin Ahmed (Mwanafunzi wa Sayyid Omar bin Sumeit)
4. Mzee Mwita
5. Sheikh Fatawi bin Issa
6. …
7. Sayyid Ahmed Mansab (Nyuma yake Sayyid Ahmed Hussein Badawy)
8. Sayyid Muhammad Bunamay
9. Mufti Sheikh Hassan bin Ameir
10. Sayyid Ahmad Ahmad Mwinyibaba
11. Ali Mwinyi Tambwe
12. Abbas Sykes
13. …
14. Sayyid Ahmed bin Hussein
15. Shariff Munir
16. Sayyid Abdulkadir Juneid
17. …
WALIOKAA
1. …
2. Shariff Alhardy
3. Zubeir Mtemvu
4. Issa Mtambo
5. Said Idarus
6. …
7. Sheikh Muharam Saleh
8. …
9. Sheikh Kassim Juma
10. Sheikh Ramadhani Twahir
11. Maalim Yassin
12. Mzee Himid Mbaye
13. Sayyid Ahmad Baabad
14. …

Bwana Abbas anayo picha hii katika Maktaba yake kaitundika ukutani na mimi kwa mara ya kwanza niliiona kwake lakini haikuwa na majina.

Anasema siku moja yuko nyumbani kwake Mtaa wa Shaaban Robert ghafla likaingia basi limewabeba masheikh.

Zuberi Mtemvu akateremka akamwambia kuwa kaja na masheikh wamekuja kumtembelea na kumuombea dua.

Sijaweza kufahamu hadi leo kulikuwa ba shughuli gani iliyowakusanya masheikh hawa wote Dar es Salaam.

Bwana Abbas anasema haraka akaingia chumbani kubadili nguo tayari kuwapokea wageni wake.

Ilikuwa ndiyo kwanza Abbas Sykes ameteuliwa na Rais Nyerere kuwa Regional Commissioner wa Jimbo la Mashariki.


 
Unataka kumaanisha nini Mkuu? Hivi ukifanyiwa Dua ndo unaenda peponi moja kwa moja?
 
Unataka kumaanisha nini Mkuu? Hivi ukifanyiwa Dua ndo unaenda peponi moja kwa moja?
Bio...
Sijui hayo uliyoandika yanaingiaje na hii post.

Umeuliza maana yangu.

Pili umeuliza pepo tena kwa kusubiri au kwa haraka.

Nashindwa kukupa jibu kwa kuwa sijui kama hii ni kejeli au unatafuta kujua.

Ala kuli hali swali lako hapa si pake.
 
Bio...
Sijui hayo uliyoandika yanaingiaje na hii post.

Umeuliza maana yangu.

Pili umeuliza pepo tena kwa kusubiri au kwa haraka.

Nashindwa kukupa jibu kwa kuwa sijui kama hii ni kejeli au unatafuta kujua.

Ala kuli hali swali lako hapa si pake.
Sio kejeli natafuta kujua ili nielewe toka kwako mkongwe wa muda mrefu
 
Nyerere alijitahidi kuwapa shavu aliopigania nao uhuru.
Kumbe balozi alikuwa mkuu wa mkoa.
 
Back
Top Bottom