Uchaguzi 2020 Masheikh wa BAKWATA waanza kumpigia Kampeni Dkt. Magufuli waziwazi bila aibu

Uchaguzi 2020 Masheikh wa BAKWATA waanza kumpigia Kampeni Dkt. Magufuli waziwazi bila aibu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Katika kile kinachoonekana ni unafiki wa dhahiri wa BAKWATA, Masheikh wa BAKWATA wameanza kutumia podium mbalimbali za hadhara kumfanyia kampeni Mgombea uraisi wa CCM.

Wiki kadhaa zilizopita Sheikh wa BAKWATA wa mkoa wa Dar es salaam bwana Alhadi, alionekana kung'aka na kumshambulia Muinjilisti Mwingira kwa madai kuwa anafanya kampeni madhabahuni, lakini haikupita hata miezi mitatu Sheikh huyo anasimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kutumia jina la dini kumpigia kampeni Mgombea uraisi wa CCM.

Tofauti na Askofu Bagonza na Mwamakula ambao wao huombea mikutano bila ya kuwaambia wananchi wamchague nani, huyu sheikh wa BAKWATA wa Dar es salaam amekwenda mbali na kupiga kampeni kabisa kuuombea kura mgombea huyo wa CCM.

Wakati huohuo, Sheikh huyo wa BAKWATA wa mkoa wa Dar es salaam amewashangaza sana Waislamu kwa kwenda kinyume kabisa na Imani ya dini ya dini hiyo kwa kufanya maombi kwa jina la Yesu kitu ambacho ni marufuku na ni kufuru kubwa sana kwa mujibu wa dini hiyo. Katika dini ya Uislamu inapaswa kuomba kwa Jina la ALLAH(Mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi) peke yake na si kwa jina la Kiumbe yeyote hata awe nabii au hat Malaika. Kwa mujibu wa dini ya Kiisamu Yesu ni nabii na Siyo Mungu.

Kauli hiyo imedhihirisha kuwa Sheikh huyo anaweza kufanya lolote hata kufanya kufuru ya wazi ilimradi awe karibu na watawala.

Kitendo cha Sheikh Alhadi kusema kuwa anaomba kwa jina la Yesu, kisha baadae kutamka Bismillah Rrahmaani rrahiim (yaani kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema) anaimply kuwa Jina la Allah ndiyo Jina la Yesu kitu ambacho ni kufuru kubwa sana kwa muislamu kuifanya.

Matendo haya ya BAKWATA kushindwa kulinda misingi ya dini ya uislamu yanaendelea kujitokeza mara kwa mara na yamekuwa yskiwakera waislamu wengi.

Ni wajibu wa Sheikh Mkuu na waislamu kiujumla kuchukua hatua maana hii tabia ya Masheikh hawa kuvunja misingi ya waziwazi ya dini ya kiislamu kwa sababu ya maslahi machache ya dunia yatapotosha watoto wa kiislamu na waislamu wengine kuikosa Tawhidi ya kweli.

Kama Alhadi alidhani waislamu watampa kura mgombea wa CCM kwa kufanya kufuru ya wazi namna hii basi ndiyo kwanza kamharibia!


Bakwata.JPG
 

Attachments

  • VID-20201015-WA0101.mp4
    3 MB
Huwenda itakuwa ushawishi kuwatoa mashehe ndani iwapowatachelewa lisu kasema anawatoa siku hiyohiyo kwamatamshi yake niuonezi
 
Tujiulize jambo moja, nini hatma ya BAKWATA baada ya CCM kutoka madarakani?

Ni wazi itajifia na vyombo vingine vya waislamu halisi vitachukua hatamu zake. Mambo ya fix fix ndio basi tena, waislamu sasa waheshimiwe
 
President you have been in power for 5 years your deeds should be campaigning for you without the need to even speak if you are that good a leader but alas we shall blame someone for your actions right? Still applying colonial rhetoric in the 21st century
 
Back
Top Bottom