Mashimo ya choo yasiyo jaa (Biodigester)

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
Hivi ni kweli mashimo haya ya Biodigester hayajai milele.

Na suala la harufu kuwa hayarudishi ndani ni kweli au lugha za biashara tu.

Mwenye uzoefu ama ni fundi au anatumia kwake atuhabarishe.
 
A Bio- Digester Toilet system is a Morden toilet system that does not get full . We use micro bacterials in process of the Bio Toilet digester which feed on the human waste to survive and they multiply from 1 to 100,000 within 24 hours.

The new Bio Digester have many Advantages (benefits)over the old man hole or septic tank.
These are some of the advantages

1. It saves more money as compare to the cost in constructing a septic tank

2. It’s uses small area space to produce a bio digester toilet

3. It’s Green and pure

4. No more waste removal as the micro organisms eat the waste

5. It last as long as ur building last

6. No Maintenance

7. Quick and Easy installation

8.no more files from manhole

9 odourless

10.the waste water can be use as fertilizer for ur garden and farms

~Also we Do Gray water Treatment
~Also we do water treatment and water Quality testing
 
Hivi ni kweli mashimo haya ya Biodigester hayajai milele.

Na suala la harufu kuwa hayarudishi ndani ni kweli au lugha za biashara tu.

Mwenye uzoefu ama ni fundi au anatumia kwake atuhabarishe.
Ni kweli nami natumia kwa miaka 2 sasa na sijaona changamoto yoyote, mbali ya hao wadudu micro bacterials, kiuhalisia uchafu huwa unapelekwa kwenye shimo lilifunikwa kwa udongo mfano wa tuta kubwa la viazi, ndani mawe hujazwa na yanafunikwa na nylon sheet. Hivyo kwa lugha rahisi Yale majimaji taka hunyonywa na kupotelea ardhini maana shimo lile huwa halijengewi.
 
sawa, ndio hadi milele ?
 
Hivi ni kweli mashimo haya ya Biodigester hayajai milele.

Na suala la harufu kuwa hayarudishi ndani ni kweli au lugha za biashara tu.

Mwenye uzoefu ama ni fundi au anatumia kwake atuhabarishe.

Inategemea na eneo/udongo. Asikudanganye mtu eti hayajai, yanajaa ila kama udongo ni kichanga yale mawe yana kunywa hayo maji na mawe kuyazamisha chini ardhini ndio unaona hayajai ila siku kuna mvua kubwa na choo kishajaa yale mawe mzigo unaibukia juu. Kule kunduchi beach na ununio mafundi waliweka hivyo saa hivi wanatafutwa wamekimbia. mzigo unaelea juu kaa bahari
 
UONGO, Ni maneno tu ya kibiashara. Mimi ni fundi ujenzi na siamini ktk hilo.
Kiufupi kujaa kwa shimo inategemea na msongamano wa makazi na aina ya udongo. Maji hua yanaingia (kipindi cha masika) na kutoka yenyewe (kiangazi) ndani ya shimo. Hivyo ili shimo lijae maana yke ardhi yote ya nje inayozunguka hilo shimo iko saturated (can't hold more liquids). Nimejenga mashimo ya temporary ya ft5 au 6 tu, na almost 10yrs now hata nusu hayajafika.
 
Hata mimi ninatumia huo mfumo na naelekea kumaliza mwaka toka nianze kutumia na kimsingi Hadi muda huu sijaona changamoto yoyote!
Kuna kuwa na mashimo mawili ambapo shimo Moja ni kwaajili ya Maji taka Yale ya kuogea na yanayotoka jikoni ambayo yanakuwa na chemicals za Sabuni za kuogea na kuoshea vyombo. Haya Maji Huwa yanaelekezwa kwenye shimo kubwa kidogo lililojazwa mawe na kufukiwa.
Na shimo la pili hili Huwa limejengwa Kwa zege na linafunikwa na ndiyo linalowekwa hao bacteria ambao husaidia kula kinyesi. Na shimo hili Huwa halitakiw kuelekezwa na Maji ya bafuni na jikoni kwasababu ya Maji yake ambayo yana chemicals ambao wanaweza kuua wale bacteria.
 
Well [emoji1666]
 
Ni kweli nami natumia kwa miaka 2 sasa na sijaona changamoto yoyote, mbali ya hao wadudu micro bacterials, kiuhalisia uchafu huwa unapelekwa kwenye shimo lilifunikwa kwa udongo mfano wa tuta kubwa la viazi, ndani mawe hujazwa na yanafunikwa na nylon sheet. Hivyo kwa lugha rahisi Yale majimaji taka hunyonywa na kupotelea ardhini maana shimo lile huwa halijengewi.
Hao wadudu wanawapandikizaje humo au wanatokea wenyewe?
 
Back
Top Bottom