Mashindano ya CAF ngazi ya makundi kwa vilabu 2022/2023

Mashindano ya CAF ngazi ya makundi kwa vilabu 2022/2023

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Habari wadau wa JF. Naomba mupokee na kuendelea kuboresha hili bandiko linalohusu mashindano ya CAF kwa vilabu kwa msimu wa mwaka 2022/2023. Kwa kuanzia nitaweka misimamo kwa mashindano tajwa ambapo nitawaomba wadau muanze kutoa tathmini zenu bila matusi kuangalia mafanikio ya vilabu toka katika zile nchi (Moroko, Tunisia, Algeria, Misri,Afrika kusini na DRC Kongo) ambazo vilabu vyake vimekuwa vikitawala soka la Afrika.

Itakuwa vyema tukianza kutabiri kwa kutoa sababu kama nchi tajwa hapo juu vilabu vyake vitaendelea kutawala au kutakuwa na vilabu vya nchi zingine zinazoweza kuleta mapinduzi (surprise). Bila kujali mirendo ya Usimba na Uyanga unadhani nini nafasi ya vilabu vyetu kwenye mashindano tajwa hapo juu na nini kifanyike kuanzia mwaka huu ili vilabu vyetu viweze kufanya vizuri Zaidi kwenye haya mashindano.

Wadau wa JF karibuni​

CAF CHAMPIONS LEAGUE
CHAMPION LEAGUE.png


CAF CONFEDERATION CUP
CONFEDERATION.png
 
Mashindano ya mwaka huu yako na ugumu kwani naona hapo baadhi ya timu kubwa zimeanza vibaya, Bado nafasi za timu za afrika ya kaskazini zipo tena kubwa tu, naona timu kama Petro de Luanda wamedhamiria kabisa kufanya kitu kubwa.

Timu za nyumbani mfano Simba chaguo walilonalo Sasa ni kushinda mechi zote zilizobaki au kutoa sare Moja kwenye mechi zilizobakia kimahesabu, ila kwenye pitch timu kama Simba nafikiri ina vitu Vingi vya kufanya, Kwa kweli hatujaona ile agressivness ya Simba kabisa, mechi na horoya ilikuwa ni ya Simba kabisa kama TU kungekuwa na matumizi mazuri ya nafasi nalo hili la kutokutumia nafasi ni tatizo Moja kubwa na litaigharimu Simba pa kubwa kwenye hii tournament ya msimu huu.

Kama Simba isipobadilika kuanzia mechi ya kesho sioni ikienda popote zaidi ya kuishia makundi...Yanga wao wahakikishe nyumbani hapa ni kushinda TU, ugenini hata sare inatosha, tatizo la set pieces liliigharimu timu ugenini naamini kocha ashaliona vice versa ya hii ataadhibiwa ugenini, naiona mechi ya marudio na tp mazembe ikiwa tough.
 
Sioni simba akipita group stage timu aliyokua nayo safari hii sio ya ushindani na sidhani kama kutakua na mabadiliko yoyote uko mbeleni asipokua makini anaweza kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi lake. Upande wa yanga kuna vitu viwili anatakiwa kufanyia kazi kwanza kuja na mbinu ya kuzuia mipira mirefu inayoelekezwa golini kwake pili kutilia mkazo kwenye kumaliza mechi mapema kuliko kupiga pasi nyingi zisizo na faida. Magoli yapatikane kwanza by any means possible alafu ndio waanze kutembeza possesion ya mpira sasa
 
CHAMPION LEAGUE_VR1.png


Hii ndiyo CAF champion League 2022/2023. Hebu angalia nafasi za Wydad Ac (Mabingwa watetezi) na National Al Ahly, Je viwango vya Vilabu washiriki mwaka huu ipo juu AU viwango vya hivyo Vilabu tajwa vimeshuka?
 
CONFEDERATION_vr1.png

Hebu angalia nafasi ya vilabu vya Congo DRC kwenye CAF Confederation Cup 2022/2023, Je Soka la Kongo linaelekea wapi? nini maoni yako
 
View attachment 2531789
Hebu angalia nafasi ya vilabu vya Congo DRC kwenye CAF Confederation Cup 2022/2023, Je Soka la Kongo linaelekea wapi? nini maoni yako
Kwenye soka la ndani team nyingi zina suffer kimataifa ila likija swala la kufuzu world cup au afcon wanatufunga kwasababu wenzetu wana professional wengi sana kutoka nje ndio maana unaona vilabu kama vya ghana na Nigeria havifanyi vizuri kimataifa ila kwenye national team zikikutana na Tanzania tunapigwa kwasababu ya professionalism ndio maana kwenye kipindi cha Salama alifanya na samatta alimuuliza

samata unadhani soka letu lina kwama wapi akajibu tuna kwama kwasababu hatuna wachezaji wengi professional hata hao Congo unaona team zao mbovu ila wakija kucheza Tanzania wanatupiga hamsa.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
CAF CHAMPION LEAGUE 2022/2023 : Group Stage Match 5 of 6

CAF Champion League But one.png


CAF CONFEDERATION CUP 2022/2023 : Group Stage Match 5 of 6

CAF Confederation cup 2023 last but One.png
 
Kwenye CAF Champions League tayari timu SABA kati ya NANE zitakazoingia Robo Fainali zimejulikana ambapo timu ya NANE itaamuliwa na mchezo baina ya Al Ahal ya Miiri na Al Ahal ya Sudan mchezo utakaochezwa huko Misri. Bila kujali matokeo ya mechi baina ya Al Ahal ya Miiri na Al Ahal ya Sudan kwa mwaka 2022/2023 robo fainali itahusisha timu Sita juu ya Jangwa la Sahara na timu mbili tu toka chini ya jangwa la sahara kama inavyoonekana hapa chini

Morocco – Timu Mbili

Algeria – Timu mbili

Tunisia – Timu Moja

Tanzania – Timu Moja

Afrika kusini- Timu Moja

Sudan/Misri- Timu Moja

Katika mashindani ya CAF Champions League 2022/2023 Ngazi ya Robo Fainali yanaweza kukosa timu toka Misri kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka Zaidi ya Ishirini iwapo matokeo baina ya Al Ahal ya Miiri na Al Ahal ya Sudan yataisha kwa sare au timu toka sudan kushinda. Hatua hii kukiwa kumebakiwa na Mechi moja katika ngazi ya makundi tayari washindi wa kwanza na wapili wameshajulikana isipokuwa mshindi wa pili kundi B. Je hii ina maana gani? Mashindani ya CAF Champions League 2022/2023 ni marahisi sana au magumu sana kiasi cha Mafuta na Maji kujitenga kwa urahisi? Nani anaweza kuwa Bingwa kwa mwaka huu? Je ni uwekezaji wa aina gani unatakiwa kufanywa na Timu za nchi chini ya Jangwa la Sahara ili kuweza kushindani na timu toka Nchi za kiarabu Kaskazini mwa Afrika?
 
Katika mashindano ya CAF Conederation cup 2022/2023 ikiwa kumebakiwa na mechi moja tu kwa kila Kundi ni Group B na D ambako timu mbili zitakazoingia Roba Fainali zimeshajulikana na katika Group C ni timu moja tu imeshajulikana. Kwa picha hii inaa maana timu tatu za kuingia Robo Fainali ya CAF Conederation cup 2022/2023 zitajulikana katika Mechi za mwisho (Group Stage). Je hii ina maana gani ukilingalisha na mashindano ya CAF Champions League 2022/2023? Nani anaweza kuwa Bingwa wa mashindano ya CAF Conederation cup 2022/2023 kwa mwaka huu? Je unaonaje uwakilishi wa timu za Nchi chini ya Jangwa la Sahara katika haya mashindano
 
Sioni simba akipita group stage timu aliyokua nayo safari hii sio ya ushindani na sidhani kama kutakua na mabadiliko yoyote uko mbeleni asipokua makini anaweza kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi lake. Upande wa yanga kuna vitu viwili anatakiwa kufanyia kazi kwanza kuja na mbinu ya kuzuia mipira mirefu inayoelekezwa golini kwake pili kutilia mkazo kwenye kumaliza mechi mapema kuliko kupiga pasi nyingi zisizo na faida. Magoli yapatikane kwanza by any means possible alafu ndio waanze kutembeza possesion ya mpira sasa
Huna hata aibu baba zimaa kuandika hiviii, simba inakutesaa sanaaa? Km umeumizwa na matokeo ya simba kuingia robo kibabeee, kunya bogaa, mbwehaaa wee.
 
Back
Top Bottom