Mashindano ya Olimpiki: Tanzania kupeleka wanariadha 3 tu?

Mashindano ya Olimpiki: Tanzania kupeleka wanariadha 3 tu?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Aiseee sijui kama tuko sawa au kuna shida sehemu. Nilisikitisjwa sana juzi kusikia kwamba Tanzania itapeleka wanariadha watatu pekee kule Tokyo Japan.

Hii ni ajabu sana na sijajua tunakwama wapi sisi.

Kadri miaka inavyo songa mbele ndivyo tunavyo kosa u seriouse, na tunavyo endelea huenda tusipeleka hata mwanariadha mmoja.

Shida ni viwango hakuna au nini?

Ka vipi tuajiri viongozi kutoka hata Kenya waje kuinua viwango.
 
Kwa mfuatiliaji mzuri wa michezo hasa riadha, atakubaliana nami kwamba wachezaji watatu wa kitanzania waliofanikiwa kufuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki 2021 yanayotarajiwa kutimua vumbi kati ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu, wanayo nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo na kuletea taifa heshima. Nimefuatilia wachezaji hawa mazoezi yao na kujiridhisha kwa upande wao wanajitahidi kadiri Mwenyezi Mungu alivyowajalia kuhakikisha wanakua kwenye ubora utakaowapa nafasi ya kufanya vizuri. Hata hivyo, wachezaji hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi zisizohusiana na masuala ya kiufundi bali zinazohusiana na siasa za viongozi wa wizara na chama cha Riadha Tanzania – RT.
Chama cha Riadha Tanzania, mnamo mwanzoni mwa mwezi Machi 2021 walizindua kambi kwaajili ya wachezaji hawa. Kambi hii imekua ikisimamiwa na kiongozi mmoja tu, ndugu John Bayo. Bwana Bayo ndie yule kiongozi anaelalamikiwa kutokua na sifa za kushika nafasi ya Umakamu wa Rais wa RT anayoishika. Tetesi zinasema, ndugu huyu hakuwahi hata kumaliza kidato cha nne kwani shule ya seminary iliopo mkoani singida ambapo alihudhuria elimu ya sekondari, ilimtimua akiwa kidato cha tatu baada ya kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi ya jirani na seminari hiyo. Bayo huyu aliwahi kua Diwani wa Chadema alietimuliwa na chama hicho kwa tuhuma kwamba amepokea rushwa ya shilingi milioni kumi na kuuza kura yake wakati wa sakata la uchaguzi wa Meya wa jiji la Arusha mnamo mwaka 2011.
Tangu kambi hii ianzishwe, wadau mbalimbali wamekua wakilalamikia namna inavyoendeshwa kuanzia uchaguzi wa wachezaji mpaka utaratibu wa manunuzi Bayo aliwah kusemwa na bwana Gidabuday kwenye kipindi cha ITV kwamba ndie anaeenda mpaka kununua nyanya sokoni kwaajili ya kambi. Makamu wa Raisi wa chama cha kitaifa aseye na sifa inabidi akanunue nyanya kwakua hajui hasa ukubwa wa nafasi yake hiyo na anadhani amechaguliwa ili akanunue nyanya na Tangawizi badala ya kuwaza sera zinazoleta maendeleo ya kweli kwenye riadha.
Wakati wa uzinduzi ilielezwa kwamba kambi hiyo ilikua ni kwaajili ya kuwapa wawakilishi wa nchi kwenye Olimpiki fursa ya kufanya mazoezi, pamoja na wale waliokua na ubora ambao ungeweza kuwafanya wafuzu kwa michuano ya Olimpiki. Bwana Bayo alikusanya makocha wa Arusha wa kabila lake tu la wa Mbulu kasoro kocha mmoja, na kukaa nao katika ukumbi wa uwanja wa Shehe Amri Abeid jijini Arusha na wakachagua wachezaji kumi na nne ambao asilimia kubwa ni wa kabila lake la wambulu kasoro Alphonce Simbu na hakukua na hata mchezaji mmoja kutoka nje ya mkoa wa Arusha/Manyara. Uteuzi huu wa wachezaji wa kukaa kambini kwa gharama za RT haukushirikisha kiongozi mwingine yoyote wa RT wala wa chama mkoa zaidi ya katibu na mweka Hazina wa chama cha Riadha Mkoa wa Arusha bwana Tomas Tlanka ambae baadae alikuja kumchagua kua kocha wa Timu ya Olimpiki atakae safiri na Timu kwenda Japan na wachezaji. Watu wengine waliohudhuria kikao hicho ambacho hakikutangazwa na kuwekwa wazi kufanyika kwake walikua ni makocha ambao wote wanatoka kabila lake kasoro kocha mmoja tu ambae amempa ukocha msaidizi kwa kile ambacho mara kadhaa amesikika akisema ili isionekane amejaza wambulu tupu. Kocha huyu msaidizi ni nunge asiekua na analojua zaidi ya kwenda nae sokini kubeba viazi, nyanya na tangawizi.
Baada ya uteuzi huo wa lundo la wachezaji wanaokaa kambini bila kua na malengo na haijulikani wanakusudia kufanya nini zaidi ya kuongeza gharama kwenye chama, bwana Bayo kinyemela amekua akiongeza idadi ya wachezaji bila kushirikisha mtu yoyote huku akipokea pesa kwa manufaa yake binafsi kutoka kwa wazazi na mameneja wa wachezaji mbalimbali wakati wakikaa kambini kwa gharama za chama na sasa idadi ya wachezaji imefikia zaidi ya ishirini na kuna kila dalili ikaendelea kuongezeka. Wingi huu wa wachezaji waliojazwa bila malengo wala maamuzi ya kamati husika na maswala ya ufundi, unaenda kinyume na kanuni za kujikinga dhidi ya Kovid19 ilizotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa na serikali ya Japan. Kwa kutambua hilo, baada ya kambi kukabidhiwa kwa Kamati ya Olimpiki, Kamati ya Olimpiki Tanzania imeamua kuhamisha wachezaji watatu waliofuzu na kuwapeleka kwingine ili kuwaepusha na uwezekano wa kupata maambukizo ya kovid na kuinyima nchi uwakilishi. Kwa sasa, wachezaji hao wamehamishiwa kwingine na ile kambi ya RT imebaki na wachezaji ambao hawajulikani Kamati ya Ufundi ya RT ilikaa lini ili kuamua kuhusu uwepo wao huo. Idadi kubwa ya wachezaji waliobaki kambini hapo ni wale ambao Bayo alipokea hela ama kwa wazazi ama mameneja ili awaweke kambini kwa gharama za RT. Bahati mbaya, Rais wa RT bwana Silas Isangi ana imani kubwa sana na Bayo na kumuachia kila kitu kuhusu kambi hiyo.
Changamoto ya pili ambayo wachezaji hawa wanakumbana nayo, ni uwezo mdogo wa kiufundi walio nao makocha wanao wasimamia mazoezini. Makocha hawa ni Tomas Tlanka na Anthony Mwingereza. Kocha aliekua amechaguliwa kihalali na uongozi wa RT uliotoka madarakani, na kubarikiwa na uongozi wa sasa ni Francis John na Mwaka Mrisho kutoka Zanzibar (ili ku balance Tanzania Bara na Zanzibar), Francis John ni kocha wa muda mrefu ambae aliwahi kuwa Rais wa RT kabla ya Anthony Mtaka. Kocha huyu ana viwango vya kimataifa, na miaka kadhaa amekua kocha wa timu ya taifa Tanzania. Kinyume chake, kocha Tomas Tlanka ni mlevi wa kunywa pombe nyingi bila kujali ni muda gani, lakini zaidI uwezo wake kiufundi ni wa hali ya chini mno. Bayo alipoingia madarakani alihakikisha anamtoa Kocha Francis kwa sababu kwanza ni mtu anaemzidi elimu na uzoefu katika usimamizi wa mchezo wa riadha na hivyo isingekua rahisi kwake kufanya madudu yake ya kujaza wachezaji kambini kwa manufaa yake, na labla aliona kambi ingeendeshwa kitaalam na hivyo yeye kujikuta hana nafasi ya kupiga.
Mbali na hatari ya kuzuiliwa kutokana na kukiuka kanuni za kujikinga na maambukizi ya kovid, wachezaji hao wanakabiliwa na changamoto ya uwezekano wa kupoteza faida ya kufanya mazoezi kwenye uwanda wa juu. Arusha iko uwanda wa juu ambao ni faida kwa wachezaji. Na wataalamu wanasema, mchezaji anapoteza faida ya uwanda wa juu iwapo atakaa kwenye uwanda wa chini (See level) kwa zaidi ya siku nane. Ukifuatilia utagundua nchi ambazo ziko makini na wachezaji wake zimewaweka kambini katika uwanda wa juu, nchi hizi ni pamoja na Japan yenyewe, Kenya na Ethiopia. Wachezaji wa Kenya wanaoshiriki marathon wamepanga kuelekea Japan mnamo tarehe 03 mwezi wa nane ambapo watakaa japan kwa siku tano tu kabla ya kukimbia mnamo tarehe 08 mwezi wa 08. Lakini sisi, kwasababu za ubinafsi tatizo lilianzia kwa Mkurugenzi wa Michezo Dr. Yusuf Singo ambae ili akusanye posho za kutosha kutoka serikalini aliamua timu iondoke Tanzania na kwenda kuweka Kambi Japan kwenye mji wa Nagoya kwa mwezi mzima kabla ya mashindano. Dr. Singo alikutana na upinzani mkubwa kwenye sakata hili hasa kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Olimpiki ndugu Fiilbert Bayi ambae alikataa timu kwenda Nagoya kwa mwezi mzima. Baada ya kukwama aliamua kumuandikia barua katibu huyo kumpa malekezo kwamba serikali inataka timu iende kambini Nagoya. Bayi alipuuza maelekezo hayo na kueleza kua Timu itaondoka kwenda Japan mnamo tarehe 29 Julai. Hata hivyo, masuala ya kiitifaki yatakua kikwazo kwa wachezaji hawa kwani wanapaswa kuja jijini Dar tarehe 24 mwezi Julai. Ukifanya mahesabu utagundua tarehe 24 mpaka tarehe 08 agosti siku ya marathon, wachezaji hawa watakua wamekaa kwenye uwanda wa pwani kwa zaidi ya siku kumi na sita na hivyo kupoteza kabisa faida ya kufanya mazoez kwenye uwanda wa juu. Zaidi ya hapo, kwa siku hizi zote haiweleki mpango gani umewekwa kuwasaidia wachezaji hawa kuendelea kufanya mazoezi yao.
Nina matumaini makubwa, viongozi wa serikali wanaohusika watachukua hatua na kuhakikisha angalau wachezaji hawa wanaondoka Tanzania si chini ya tarehe moja ya mwezi wa nane na kutoka Arusha angalau tarehe 29 mwezi wa saba. Sababu za kung’ang’ania waondoke mapema inasemekana ni mipango ya kununua tiketi kwa kikundi ambapo italeta unafuu. Labla tuangalie kama tutaweka rehani ari ya wachezaji hawa na uwezekano wao kuweka kumbukumbu ya maisha kwa kuchukua medali ya olimpiki na kuletea heshima taifa kwa sababu ya kuokoa dola chache za tiketi?
Mwisho ninaomba wasaidizi wa mama Samia Suluhu Hasan waangalie utendaji wa Dr. Singo kama anatendea haki nafasi yake ya Ukurugenzi wa Michezo nchini, lakini pia na utendaji wa Katibu wa BMT na kumshauri mama ipasavyo. Nionavyo mimi, Waziri wa Michezo atakuja kuponzwa na viongozi hawa.
Pia itazamwe idadi ya maafisa wa serikali wanaotarajiwa kusafiri na timu, na kama kuna ulazima wa maafisa wa serikali kusafiri na timu hasa ukizingatia gharama za serikali zitakazotumika pasipo sababu ili hali tuna maafisa wa Ubalozi wetu Japan.
 
Back
Top Bottom