Mashindano ya Olimpiki yameisha?

Mashindano ya Olimpiki yameisha?

ntuchake

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
408
Reaction score
1,549
1724228076892.jpeg

Wakuu kwani mashindano ya olimpic yameisha? Kulikuwa na nyuzi tele humu za kuwafagilia watanzania walioenda kwenye mashindano. Mlikua mna mbwembwe wakati mnaenda ila sasa hivi kimyaaa 😂😂

Pia soma: Mwanariadha Alphonce Simbu amaliza nafasi ya 17 Olimpiki Jijini Paris, Ufaransa

Hiki kimya chenu inaonekana kabisa mlishindwa. Hamkuambulia hata medali ya shaba 😂 Mngeshinda ningeshangaa. Watanzania na michezo wapi na wapi. Sie tukalie majungu na uchawi kurogana ili tusiendelee hayo mengine tuwaachie wakenya, Rwanda na Uganda!
 
Kweli wameshindwa ila kuna Makandokando Mengi kwenye kamati ya Olimpiki Tanzania, Wachunguzwe
 
Ukiona mqshindano hakuna hata motosha kutoka kwa wanasiasa kama yale ya CAF ,champions legue ujue hao walikuwa wanaenda kujaribu bahati yao ya kutafuta Ugali.
 
Ukiona mqshindano hakuna hata motosha kutoka kwa wanasiasa kama yale ya CAF ,champions legue ujue hao walikuwa wanaenda kujaribu bahati yao ya kutafuta Ugali.
Kwani ya CAF tulishinda?!
 
Watanzania tunaongoza kwa kukatisha tamaa wanamichezo wetu. Nimepitia page za Wakenya naona wanawapongeza hata wale waliofanya vibaya, wanaamini kuna wakati watashinda.

Watanzania tunaombeana sana njaa, wengi habari ya Simbu kushindwa inawafurahisha kuliko mkisikia ameshinda. Taifa gani hili?

Naamini hakuna mchezaji anayepokea bendera ya Taifa aende kwenye mashindo makubwa kama hayo acheze chini ya kiwango. Hicho mnachoona ameonesha ndio uwezo wake wote.

Hamjawahi hata kusikia changamoto wanazopitia kuanzia maandalizi hadi ushiriki wao kwenye mashindano ila mnakuwa wa kwanza kuwakejeli wakishindwa.
 
Back
Top Bottom