DOKEZO Mashine ya CT Scan Hospitali ya Mloganzila ni Mbovu kwa zaidi ya Miezi mitatu sasa, tatizo nini?

DOKEZO Mashine ya CT Scan Hospitali ya Mloganzila ni Mbovu kwa zaidi ya Miezi mitatu sasa, tatizo nini?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naandika nikiwa na huzuni sana hapa najiuliza ni uzembe wa Serikali au Uongozi wa Hospitali ya Mloganzila ulio chini ya Profesa Janabi au Dr Magandi...

Mwaka jana 2024 nilikuja na mgonjwa wangu akihitaji huduma ya CT Scan lakini cha kushangaza nikaambiwa huduma haipatikani hapa mpaka Muhimbili ya Upanga...

Kuuliza sababu naambiwa ni mbovu na wanafanya mchakato wa kuitengeneza, cha kushangaza ni zaidi ya miezi mitatu sasa nimeulizia pale naambiwa bado haijatengamaa...

Je, kuna mchezo mchafu wa hujuma unafanyika? Inawezekanaje Hospitali kubwa ya Rufaa yenye Hadhi ya kimataifa kama Mloganzila kukosa Huduma ya CT Scan?

Halafu hii sio mara ya kwanza kuripotiwa humu, sasa na leo napaza sauti Wahusika wa Wizara ya Afya na Wasaidizi wa Rais nendeni kachunguze kuna mchezo mchafu unaendelea pale Wananchi kukosa Huduma hii ya msingi na kuanza kupanga foleni kujazana zaidi ya wagonjwa watano kwenye Ambulance moja kwenda Muhimbili Kubwa sio sahihi na ni usumbufu kweli...

Mheshimiwa Rais anatoa fungu zuri tu kwa ajili ya mambo ya Afya lakini kuna Watendaji wanamuangusha, Wahusika wa Mloganzila Hospitali, oneeni uchungu kodi za Watanzania!

Soma pia: DOKEZO - Mashine ya CT-SCAN katika Hospitali ya Mloganzila ni Mbovu
 
Maghufuri ndo alikuwa anawapenda watoa taarifa kama wewe.
 
Back
Top Bottom