Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,903
- 1,360
Wewe unapatikana wapi? kama uko Dar es salaam tuwasiliane kupitia 0655746067
Naoma msaada wenu wadau.
Nina mpango wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji, natakiwa kusukuma/kuvuta maji kwa umbali wa mita 250 (hakuna mwinuko mkubwa) halafu niyapandishe juu urefu wa mita 6 ili yaingie kwenye simtank, tayari kwa umwagiliaji.
Eneo langu linweza kufikia eka 6. Je ninunue mashine yenye ewezo gani (HP), kama kuna anayejua aina nzuri ya mashine naoma anisaide pamoja na bei pia upatikanaji wa spares ni muhimu.
Asanteni
tafuta honda 5.5HP, 3inch (HONDA W30XT)
Hapana, nataka kumwagilia kwa kutumia mipira ya kawaida au ikiwezekana sprinklers, Sababu ya kutaka kuyapandisha kwenye tanki juu, ni kupunguza uwezekano wa kuwasha mashine kila unapotaka kumwegilia (tank linakuwa kama storage fulani, yakiisha ndio nasukuma mengine)Natumia nchi mbili ila haina pressure kubwa sana,kupandisha maji juu ya tanki.unafanya umwagiliaji kwa njia drips?
Kama hiyo inchi mbili haina pressure sana, itaweza kuyapandisha kwenye tank?Natumia nchi mbili ila haina pressure kubwa sana,kupandisha maji juu ya tanki.unafanya umwagiliaji kwa njia drips?
Pia tujulisha upatikanaji wa spares, maana mashine nyingi za kijapan spares ni shida, angalia kwa mfano pikipiki honda XL 125s, Spares za shida sanaMkuu unaweza kujua bei yake inaanzia ngapi.
Habari yako ndugu,
Ndugu swahili lako halijajitosheleza inaweza ikawa ngumu kupata msaada.
1.Ili kujua usaidiwe vipi nipazima kujua chanzo chako cha maji, namaana hayo maji unayotegemea kutumia kwa kilimo unayatoa wapi? Sababu pump unayoweza kutumia kutoa maji mtoni au kwenye bwawa tofauti na pump ya kisima cha kudumbukiza.
2. Angalia umbali kutoka chanjo cha maji.
3. Nishati gani utatumia kuendeshea pump hiyo. ( umeme, mafuta, soral nk)
4. Mfumo gani gani unatumia kwa kumwagia but hilo sio muhimu sana.
Utakaporudi na majibu ya haya tunaweza kumushauri vizuri zaidi.
sh ngap mkuuNipe pesa nikuuzie ninayo mkuu nimeinunua mwaka jana nikaitumia kulima misimu miwili ya tikiti basi.
Njoo pmsh ngap mkuu
Asante kwa maelezo, Nataka pump ya katoka kwenye mto kuja shambaNdugu maelezo yako hayajajitosheleza. Inamaana unahitaji pump? Kama ndio kuna aina 2 za pump ya juu ya ardhi na chini ya ardhi ili kuzitofautisha pump hizi nilazima tujue chanjo cha maji kwenda shambani.
Kama utakuwa unatumia chanzo cha maji kama bwawa, rambo, mto au kisima kisichozidi kina cha 8 mpaka 10 unaweza kutumia pump za kawaida tu ambazo kariakoo zipo kaushiki, honda na nk, ambapo ukienda dukani mara nyingi watakuuliza ni nchi moja nanusu au nchi 2.
Hapo kuna namna mbili unaweza ukatumia moja kwa moja wakati wakati unavuta maji ukamwagia kwa wakati huo huo. Nawengine wanatumia njia hii kwenye mfumo wa drip irrigation.
Njia yapili kama unatumia mfumo wa drip irrigation kwanjia ya gravit itakulazimu hayo maji yatakapokuwa yanatolewa kwenye chanzo kwenye matank yalio juu usawa wa mita 3 mpaka 4 kutegemeana na ukubwa wa eneo la umwagiliaji ili utakapotaka kumwagilia maji yashuke kwa gravit.
Pump nyingine ni pump za chini ya ardhi hizi hutumika kwenye vyanzo vya maji vilivyo chini ya ardhi ninamana visima virefu. Hapa sina maelezo sana sababu maelezo yake nikama hayo mengine niliotoa huku juu.
Ndugu nimekupa mwanga kidogo utakaporudi tena kufafanua vizuri unachohitaji. Pia watakuja wajuzi zaidi kukupa maelezo yakutosha na kunirekebisha au kunikosoa pale nilipokosea.
Nakutakia kila lakheri na mafanikio.