Mashine za EFD na 18%

bolsto

Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
36
Reaction score
5
Habari zenu wana jamii,

Kuna swala nakutana nalo kila siku. Wafanyabiashara wengi wanadhani ya kwamba wakianza kutumia mashine wanakatwa kodi 18%. Jambo hili sio hapa Dar tu, hata mikoani nimekutana nalo.

Si kweli wafanyabiashara wote wanakata 18%. Kwa lugha rahisi, mashine hizi hazibadilishi mfumo wa ulipaji kodi, bali mfumo wa utunzaji kumbukumbu za mauzo na manunuzi ya mfanya biashara.

Mfanyabiasha wa kawaida ambaye hajasajiliwa kwenye VAT, hatokatatwa hiyo 18%. wafanya biashara wenye VAT tu ndio wanakatwa 18%, na walikua wanakatwa hivyo tokea hata mashine hazijaanza kutumika.

Na kuna faida yake, ndio mana hawakuwahi kulalamika phaze 1, maana wafanyabiashara wa VAT ndio walioanza kutumia mashine phaze I ambayo ilianza 2010, tena kuna ambao walikua wanaomba kabisa kutumia mashine.

kama umeingizwa kwenye VAT, ningekushauri uende TRA wakupe maelezo zaidi jinsi inavyokua. ukienda TRA watakupa ufafanuzi zaidi jinsi utaratibu wa VAT unavyoenda bila kumuumiza mteja.

By,
Chacha-0758 717754 / 0658 555903
Bolsto Solutions Ltd
 
Unaposema kuna faida zake bila kuziainisha unategemea watu wakuelewe vipi?
 
Bolsto solutions ltd si ndo kampuni inayozisambaza hizo mashine za EFD so nimekupata mkuu unatangaza biashara...kiuhalisia sikupingi hebu elezea vizuri faida za hii kitu na unafikiri ni kwa nini wafanyabiashara hawataki hii kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…